Na Mwandishi Wetu, Arusha
AFISA Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka Vijana mkoani Singida na Wananchi kwa ujumla kuwekeza katika Kilimo cha Viazi Lishe.
Ndahani ameyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akifunga mafunzo ya Kilimo cha viazi,maharage,mahindi lishe na kuyaoyaongezea thamani mazao hayo kwa Vijana 12 kutoka mkoani Singida walioenda kujifunza kwa udhamini wa Shirika la Chakula Duniani (FAO-Tanzania) Chini ya Mradi wa kuwawezesha Vijana kujiajiri katika Kilimo Biashara.
Ndahani alisema Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa inayozalisha viazi vitamu kwa wingi,lakini elimu ndogo ya wakulima juu ya uhifadhi wa mbegu za viazi,uchaguzi wa mbegu ,kilimo cha kisasa,uvunaji na uongezeji wa thamani zao hilo imekuwa tatizo,mfano mwaka jana wakulima wengi hawakupata mavuno kwa sababu ya kuchelewa kupanda viazi wakisubiri mvua za kwanza ambazo hutumika kama mvua za kukuzia mbegu ya viazi.
Kutokana na mafunzo hayo Vijana wa Singida watalima kisisa kutokana na mbegu ya viazi lishe ambavyo vina soko kubwa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vinavyowasaidia watoto,wazee na wajawazito.
Ndahani alisema endapo Vijana wa Singida wakajikita katika Kilimo cha Viazi Lishe tatizo la ukosefu wa ajira na utapiamlo litakoma katika mkoa huo ambapo amewaomba vijana kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao binafsi,moa na Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MBC, Zena Mshana alisema vijana hao wamejifunza kwa muda wa mwezi
mmoja Kilimo cha Viazi Lishe, Maharage Lishe na Mahindi Lishe pamoja na
uongezeji wa thamani wa mazao hayo na kueleza watakuwa na uwezo wa kuanzisha miradi
ya kilimo na kuwa wakulima wakubwa..
Aidha alisema wameamua kujikita katika kilimo cha mazao lishe ili kuondoa tatizo la utapiamlo ambao unawakuta watoto hasa wenye miaka 0 hadi 5.
kiongozi wa vijana hao Mvanga Juma Mohammed akizungumza kwa niaba yao ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shirika la Fao na MBC Enterprise Ltd kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa wa tija kwa vijana na kuahidi kuwa watatoa elimu kwa vijana wenzao na wakulima wa viazi na maharage lishe mkoani Singida ili kufanya kilimo chenye tija katika maisha yao na Taifa kwa ujumla kwani wanaamini kilimo pekee ndicho kinaweza kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.
Mohamed amemuomba Waziri wa Kilimo kuweka mkakati mzuri wa kuwawezesha vijana kupata mbegu ,mbolea na maeneo ya kilimo kwa vijana nchini pia TARI kuhakikisha mbegu ya Maharage Lishe Aina ya TARI 14 na 15 zinapatikana kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment