Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya bluu bahali) akipata maelezo katika banda la Huduma ya kiliniki ya biashara inayotoma huduma ya kusikiliza changamoto za wafanyabiashara kutoka taasisi za kimkakati zinazosimamia na mkukuza mnyororo wa dhamani ya biashara wakati alipotembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 -9 Desemba, 2020 kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere (SabaSaba), Barabara la Kilwa Dar es Salaam. Leo, 07 Decemba 2020 (picha na Eliud Rwechungura).
MHE. Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb), Waziri Mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara ametembelea Maonesho ya tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yenye lengo la kujenga jukwaa kwa wadau wa sekta ya viwanda, kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo katika sekta hiyo yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere (SabaSaba) tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020
Mhe Waziri mteule ameeleza kuwa lengo la kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ni kujifunza, kujionea bidhaa zinazolishwa na viwanda vyetu vya ndani, kujua bidhaa zinazotengenezwa, aina ya bidhaa hizo na kufahamu upatikanaji wa malighafi, kujua muunganiko wa uzalishaji pamoja na masoko.
“Nimepata faraja kuona mwamko mkubwa wa Watanzania kuweza kuzalisha bidhaa za Tanzania ambapo awali bidhaa hizo tulikuwa tunaagiza kutoka nje ya nchi, kupitia Maonesho nimeona dhamira yao na imenipa somo la kuona uhitaji wa uzalishaji mkubwa ili kuweza kusafirisha nje ya nchi” amesema Mhe Mwambe
Ameongeza kwa kusema kuwa nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hivyo wazalishaji wakiwezeshwa kwa kupata kipato kikubwa, wastani wa mapato utaongezeka na kuwa juu hivyo juhudi ya pamoja ndani ya serikali kuelekea mwaka 2025 nchi itaingia kwenye uchumi wa kipato cha kati cha juu utakaopelekea kuboresha maisha ya Watanzania na kutengeneza uchumi wa viwanda ulioimara wenye muunganiko mzuri kati ya wazalishaji wa kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na masoko
Amehitimisha kwa kusema kuwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara utatengenezwa mfumo thabiti wa kufanya muunganiko huo kupitia wizara zinazowagusa moja kwa moja ili kutengeza muunganiko wa wazi na matokeo makubwa na chanya
Imetolewa na;
Theresa Chilambo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-TanTrade
No comments:
Post a Comment