WILAYA YA BAGAMOYO YAPOKEA ZAIDI YA SH. BILIONI 1 KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WALENGWA WA TASAF - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 10 November 2022

WILAYA YA BAGAMOYO YAPOKEA ZAIDI YA SH. BILIONI 1 KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WALENGWA WA TASAF

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda,akizungumza juzi na  waandishi wa habari na timu ya maafisa wa TASAF waliokuwa kwenye ziara ya kuwatembelea walengwa  kuona kazi mbalimbali wanazozifanya baada ya kuwezeshwa.

Mratibu wa TASAF Wilaya ya Bagamoyo, Rose Mndeme akitoa taarifa ya shughuli za TASAF wilayani humo.

Afisa Ufuatiliaji wa Miradi TASAF, Janeth Mtelelah akizungumzia jinsi walengwa walivyokuwa wakipokea fedha hizo kwa njia ya mtandao.

Mwezeshaji wa Walengwa hao, Ally Selemani akizungumzia majukumu yao kama wawezeshaji.

Wanakikundi cha Jipe Moyowakionesha bidhaa wanazo zitengeneza baada ya kuwezeshwa na TASAF

Mlengwa wa TASAF Hidaya Mnyamisi  mkazi wa Magomeni Bagamoyo  ambaye ni mfugaji wa kuku akizungumzia mafanikio aliyopata baada ya kupata ruzuku ya uzalishaji kutoka TASAF.

Mlengwa wa TASAF Zulfa Emmanuel ambaye anauza samaki  mkazi wa Magomeni Bagamoyo akizungumzia mafanikio yake.

Mlengwa wa TASAF Sikuzani Bwana  mkazi wa Magomeni Bagamoyo  ambaye anafanya biashara ya genge akizungumzia mafanikio aliyopata baada ya kupata ruzuku ya uzalishaji kutoka TASAF.

Mlengwa wa TASAF. Halima Juma ambaye anauza samaki  mkazi wa Magomeni Bagamoyo akimuhudumia mteja wake.

Mlengwa wa TASAF Halima Juma akiwa amesimama mbele ya nyumba yake anayoishi.

Mlengwa wa TASAF Halima Juma akiwa amesimama mbele ya nyumba yake mpya aliyosaidiwa kupaua na TASAF.

Mlengwa wa TASAF Halima Jumanne ambaye ni mama lishe akiwajibika kwenye ofisi yake.

Mnufaika wa TASAF  Elizabeth Stephano akiwa kwenye duka lake alililozianzishabaada ya kupata ruzuku ya uzalishaji toka TASAF.

 Mume wa Mnufaika wa TASAF Hawa Diwani,  Abdallah Lukange Lukange ambao wanafanya kilimo cha mbogamboga na mpunga akielezea mafanikio waliyonayo baada ya kupata ruzuku ya uzalishaji kutoka TASAF.

Moja ya bustani ya mbogamboga la walengwa hao Hawa Diwani na mume wake linavyoonekana.

Mnufaika wa TASAF Mwanaheri Dalu ambaye ni mshonaji wa nguo akiwajibika.

Na Dotto Mwaibale, Bagamoyo, Pwani. 

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 imepokea zaidi ya Sh. 1 Bilioni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wilayani humo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri Selenda,alisema hayo juzi kwa waandishi wa habari na timu ya maafisa wa TASAF waliokuwa kwenye ziara ya kuwatembelea walengwa  kuona kazi mbalimbali wanazozifanya baada ya kuwezeshwa .

Alisema katika fedha hizo Sh.1.76 Bilioni walizipokea kwa ajili ya ruzuku ya uzalishaji na Sh.512 Milioni walipokea  kwa ajili ya ruzuku za kawaida na kuwa ruzuku za uzalishaji zinakwenda kusaidia kwenye shughuli za kilimo, ufugaji na biashara ndogondogo.

Alisema kwa fedha za ruzuku ya kawaida zinakwenda kusaidia kwenye maeneo mengine kama ya uvuvi na ufugaji lakini hizo milioni 620 kwa ajili ya ruzuku za uzalishaji zinakwenda kuwanufaisha  walengwa 1320 ambapo kati yao waliopata ruzuku za uzalishaji ni walengwa 1158 sawa na asilimia 88.

Selenda alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo na mchango mkubwa inaoutoa kwa wilaya hiyo na kuwa wao kama viongozi wajibu wao ni kusimamia na kuona wananchi wanaikuza mitaji yao kwa ajili ya kupata maendeleo.

Mratibu wa TASAF Wilaya ya Bagamoyo, Rose Mndeme alisema wilaya hiyo ina jumla ya kata 11 na kuwa vijiji 26 vipo kwenye mradi wa TASAF vyenye walengwa 3056 ambao wanalipwa ruzuku za aina tatu, ruzukuya kawaida, kufanya kazi kwa miradi (ajira ya muda mfupi) na ruzuku ya uzalishaji.

Alisema katika ruzuku ya uzalishaji wanawalengwa 1320 ambao wamepewa ruzuku ya Sh.620 Milioni kwa ajili ya kwenda kutekeleza miradi ya ufugaji wa mbuzi , kuku, ng’ombe, kilimo cha mbogamboga, ukaangaji wa samaki na kuziuza, biashara ndogondogo kama za kuuza madera, usukaji wa mikeka na nyinginezo.

Alisema ili kusimamia walengwa hao waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kuna timu ya wawezeshaji 26 kutoka katika kata hizo 11kutoka katika idara za mifugo, maendeleo ya jamii,kilimo na afya ambao wanawatembelea waengwa hao 1320 ili kujua maendeleo yao na changamoto ambazo wanazitafutia ufumbuzi.

“Kufuatia timu hiyo abayo inakwenda kutoa ushauri wa kitaalamu katika wilaya yetu miradi yote inayofanywa na walengwa inakwenda vizuri tunashukuru Mungu hivyo tunategemea kuwatoa kwenye mpango ili waweze kuwapisha watu wengine kwa kuwa sasa wameweza kusimama wenyewe” alisema Mndeme.

Mndeme alitumia nafasi hiyo kumshuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Selenda, Mkuu wa Wilaya, Zainab Abdallah  kwa usimamiaji mzuri wa miradi hiyo pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi na kuzielekeza kuwasaidia watanzania wa maisha ya chini ili waweze kujikomboa kiuchumi. 

Afisa Ufuatiliaji wa Miradi TASAF, Janeth Mtelelah alisema fedha zote zinazotolewa kwa walengwa zinatolewa kwa njia ya mitandao ya simu na njia ya benki  ambapo walisaidiwa kufungua akaunti zao na kupata fedha zao pasipokuwa na changamotozozote.

Baadhi ya walengwa waliotembelewa na miradi yao kukaguliwa ni Hidaya Mnyamisi  mkazi wa Magomeni Bagamoyo  ambaye ni mfugaji wa kuku, Zulfa Emmanuel  ambaye anauza samaki wa kukaanga,  Sikuzani Bwana ambaye aanafanya biashara ndogondogoya genge, Halima Juma, ambaye ni mkulima na anauza samaki, Hawa Diwani ambaye anasaidiwa na mume wake Abdallah Lukange ambao wanafanya kilimo cha mbogamboga na mpunga.

Wengine ni Mwanaheri Dalu ambaye ni mshonaji wa nguo na Elizabeth Stephano ambaye anajishughulisha na biashara ya duka.

No comments:

Post a Comment