WAZIRI MKUU AONGOZA NMB MARATHON 2022 ‘MWENDO WA UPENDO’...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 2 October 2022

WAZIRI MKUU AONGOZA NMB MARATHON 2022 ‘MWENDO WA UPENDO’...!

Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki ya shilingi mil 600 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa fedha zilizopatikana kutokana na mbio  za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zilizoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuchangisha matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Hospitali ya CCBRT. Akishuhudia katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna leo jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kulia) akimvisha medali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mbio  za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ kilomita tano, zilizoandaliwa na Benki ya NMB, kuchangisha shilingi mil. 600 kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Hospitali ya CCBRT.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) akiwaongoza wakimbiaji mbio za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ kilomita tano, zilizofanyika kuanzia kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya zilizoandaliwa na Benki ya NMB, kuchangisha shilingi mil. 600 kwa ajili ya kusaidia matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Hospitali ya CCBRT. Kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Ruth Zaipuna pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede na viongozi wengine wakishiriki mbio hizo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki ya shilingi mil 600 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi (katikati) fedha zilizopatikana kutokana na mbio  za hisani za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zilizoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuchangisha matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Hospitali ya CCBRT. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kushoto) wakishuhudia.

No comments:

Post a Comment