TASWIRA YA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MSALATO MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 30 October 2022

TASWIRA YA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MSALATO MKOANI DODOMA

 

Taswira ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma

Taswira ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma

Taswira ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma

Taswira ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma.

TASWIRA ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma itakavyoonekana mara baada ya kukamilika kwa Ujenzi wake ambapo leo tarehe 30 Oktoba, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la Msingi la mradi huo Mkubwa nchini.


Katika Awamu ya kwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato utakuwa na uwezo wa kuhudumia Ndege kubwa aina ya Dreamliner 787 yenye uwezo wa kubeba abiria 350. Aidha, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka na utakuwa na miundo mbinu mbalimbali kama mnara wa kuongozea Ndege, Jengo la Watu Mashuhuri, jengo la Zimamoto, mizigo, Jengo la Rais, pamoja na Karakana.


Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato Mkoani Dodoma unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024.

No comments:

Post a Comment