Jina langu ni Hadija Rajabu, binti Kanyama.
UMRI wangu ni miaka 24, nimezaliwa Julai 8, 1998 huko Majengo, Muheza mkoani Tanga na kabila langu ni Msambaa.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania sita ninaowawakilisha katika Mashindano ya Viziwi ya Urembo, Utanashati na Mitindo ya Dunia yanayofanyika Oktoba 29, jijini Dar es Salaam.
Elimu ya msingi nimeipata huko Mwanga Viziwi mkoani Kilimanjaro mwaka 2006-2015 na elimu ya sekondari nimesoma Moshi Ufundi kati ya mwaka 2016 2019.
Kazi yangu ya sasa ni mwanamitindo.
Ninapenda kuwa mwalimu wa viziwi, mitindo na utanashati na ahadi yangu kwa Watanzania nitashinda.
No comments:
Post a Comment