MBALI na huduma za viwango vya kifalme, wateja wa Benki ya NMB wamekiri kuvutiwa na mafanikio yake kiutendaji hasa kasi ya ukuaji wake ambayo wengi wamesema ni sababu ya wao kuendelea kuwa waaminifu kwa taasisi hiyo.
Kwa kuzingatia hilo, wateja hao wamesema msimu huu wanasherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja duniani kwa kutambua pia mchango wa benki hiyo na huduma zake kwenye mafanikio yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Huko Babati mkoani Manyara, wateja wa NMB walisema benki hiyo inafanikiwa pia kwa sababu ya kuaminiwa na watu wengi kitu kinachoifanya kuongoza kwa idadi ya ambao sasa hivi ni zaidi ya milioni nne na wameishukuru benki hiyo kwa huduma bora na bunifu za kisasa
Kwa mujibu wa Bi Aika Lema, vile vile NMB inawavutia wengi kutokana na uwekezaji wake endelevu kwenye miradi ya kijamii na ufadhili wa shughuli za jumuiya mbalimbali kama ilivyofanya siku kanda ya kaskazini kuadhimisha huduma kwa wateja.
KUPITIA Mkuu wa Huduma Shirikishi, Bw Valence Mtongole, NMB ilimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw Makongoro Nyerere, vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 22.
Mtongole alisema kwao Wiki ya Huduma kwa Wateja ni zaidi ya kuwaenzi watu wanaoifanya NMB kuwa benki kubwa kuliko zote nchini kwani pia ni nafasi ya kupata maoni kuhusu huduma zao na jinsi inavyoendeshwa.
Pia, Mwenyekiti wa Wajasiriamali wa Manyara, Bw Ali Said Msuya, alisema yeye ni miongoni mwa wateja wanaovutiwa na jinsi NMB inavyotengeneza faida kubwa na kurudisha sehemu yake kwa jamii.
Kati ya mwaka 2015 na 2021, faida iliyopata NMB baada ya kodi iliyopaa kwa zaidi ya asilimia 93 kutoka TZS bilioni 150 hadi TZS bilioni 290.
No comments:
Post a Comment