Mwandishi Wetu
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepiga kalenda kusikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya Halima Mdee na wenzake 18 baada ya Shahidi Hawa Mwaifunga kuugua maradhi ya mgongo. Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Cyprian Mkeha imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo na imepanga kuendelea Novemba 2,4,8,9, Desemba 6 na 7,2022.
Mapema mahakamani hapo, Mbunge Hawa Mwaifunga akijibu maswali ya wakili wa Chadema Peter Kibatala pamoja na mambo mengine alidai katika video mbili zilizochezwa mahakamani hapo ya Mnyika na Mbowe hakuna aliyewaita wao Covid 19 na kwamba katika kiapo chake yapo maneno hayo.
Hata hivyo alidai anavyofahamu yeye Covid 19 ni yeye na wabunge wenzake 18 kwasababu kiongozi wa baraza la vijana Wilaya ya Kinondoni (BAVICHA) Shabani Othuman alionekana katika video ameshika bango lililoandikwa 'kamati Kuu fukuza hao Covid 19' siku ambayo yeye na wenzake walikuwa wameitwa kuushulia kikao cha kamati hiyo.
Alidai neno Covid 19 ni muhimu katika kesi yake kwasababu ni kiambatanisho katika kesi yake na kwamba katika kesi hiyo analalamikia kutopewa nafasi ya kusikilizwa huku maneno ya Mnyika aliyotamka katika mkutano na Waandishi wa Habari yalikuwa yanawahukumu, kuleta taflani na taharuki kwa wanachama.
" Wakati nafungua kesi, madai yangu ya msingi ni kutopewa nafasi ya kusukilizwa mpaka anafukuzwa. Wakati Mnyika anazungumza na waandishi wa habari alidai hawajawahi kupeleka majina ya wabunge wateule hivyo mimi na wenzake 18 tulijipeleka, kujiapisha tukishirikiana na mfumo" alidai Hawa.
Alidai kauli hiyo ya Mnyika ilionekana tayari ameonesha maamuzi yatakayokwenda kufanyika katika Kikao cha Kamati Kuu Novemba 27 mwaka 2020. Pia alidai kwa kipindi cha miaka 14 akiwa Chadema hajawahi kuona Kamati hiyo ikitoa maamuzi pasi mshitakiwa au mtuhumiwa kuwepo au kusikilizwa.
Alidai wakati Mnyika akifanya mkutano na Waandishi wa Habari Novemba 25 mwaka 2020 alikuwa akifahamu kwamba yupo Dodoma kwasababu Novemba 24 mwaka huo ni siku ambayo waliapishwa bungeni Dodoma na wenzake 18. Alidai baada ya kupokea barua ya wito kwa njia ya Whatsapp alichofanya ni kumuomba Mnyika ampe siku saba afanye maandalizi ya kurejea Dar es Salaam kujibu tuhuma.
Awali, mahakamani hapo, Mbunge Grace Tendega aliilezea mahakama kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipendekeza majina 10 ya kuteuliwa nafasi ya ubunge viti maalum kupitia chama hicho huku akisisistiza jina la Nusrat Hanje lisikose kwasababu alikuwa maabusu.
Tendega alieleza hayo jana Mahakama Kuu ,masijala Kuu Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya wakii wake Ipilinga Panya , wakati wa usikilizwaji wa kesi aliyoifungua Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.
Tendega ambaye ni miongoni mwa wabunge alidai yeye alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) ambapo Novemba 7 mwaka 2020 kulikuwa na vikao vingi katika chama hicho ikiwemo kikao cha sekretarieti ya Bawacha ,kufanya uteuzi wa majina hayo wabunge wa viti maalum.
Alidai, wakati wakiendelea na kikao hicho Mnyika alifika akiwa na majina kumi ya wanachama aliopendekeza wateuliwe kuwa wabunge na akisisitiza jina la Nusrat Hanje liwepo kwasababu alikuwa maabusu.
"Tarehe hiyo kulikuwa na vikao vingi ikiwemo kikao cha sekretarieti ya Bawacha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum, Katibu Mkuu Mnyika alikuja na majina yake 10 na katikamajina hayo akisisistiza jina la Nasrat Hanje liwepo" alidai
Katika hatua nyingine Tendega alidai
katiba ya chama hicho haijabainisha kama Whatsapp ni moja ya njia iliyoamuliwa kufanya mawasiliano ya kiofisi isipokuwa barua pepe licha ya katiba hiyo kutambua matumizi ya Tehama.
Alidai Novemba 27 mwaka 2020 alipokea barua ya wito ya kufika katika kikao cha kamati kuu ya chama hicho na ilimfikia saa 7 mchana kwa njia ya Whatsapp huku kikao hicho kikiwa kimeshaanza asubuhi.
"Mimi barua nilitumiea kwa njia ya Whatsapp ambayo inaweza isinifikie kwa wakati kutokana na matatizo ya mtandao au usiifungue kwa wakati, ni kwelikatika kiapo changu sikuambatanisha nyaraka kuonesha siku hiyo nilikuwa wapi" alidai
Alidai ni kweli aliieleza mahakama kuwa nafasi pekee waliyopewa ni kuomba msamaha lakini unaombaje msamaha wakati hawajapewa nafasi ya kusikilizwa. Alidai hakuandika barua ya kutaka Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na Mnyika wajitowe katika kikao cha baraza kuu kilichowavua uwanachama kwasababu hawakupewa nafasi ya kufanya hivyo.
"Siku ya kikao hatukupewa nafasi ya kuandika barua ya kuomba viongozi haowajitowe, kiongozi huyohuyo alishiriki kutoa pre judgement, wangeweza kutumika viongozi wengine katika kikao cha baraza wakiwemo viongozi wa Baraza la Wazee, tungesikilizwa pengine tusingefika mahakamani" alidai.
No comments:
Post a Comment