Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa tatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria ishara ya uzinduzi wa shamba la uzalishaji kuku wazazi lililopo kwenye Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro katikahafla iliyofanyika jana Septemba 2, 2022.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi pamoja na watendaji wa shamba la uzalishaji wa kuku wazazi (Aviagen East Africa) ( hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shamba hilo uliofanyika kwenye Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, jana Septemba 2, 2022.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wawekezaji
kutoka ndani na nje ya nchi
kuwekeza katika sekta ya mifugo huku akisisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji kwa sasa hapa
nchini ni salama chini ya Uongozi wa
Rais wa jamuhuri wa muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aliyasema hayo katika uzinduzi wa
shamba la kuku wazazi la kuzalisha
babu na bibi (grand parent stock) uliofanyika wilayani siha Mkoani
Kilimanjaro jana Septemba 2, 2022.
Alisema uzinduzi wa mradi huo uliogharimu Dola za kimarekani Milioni 15
utasaidia kupanua sekta ya kuku nchini pamoja na kuongeza lishe kwa watanzania kutokana na bidhaa zitokanazo na kuku.
"Sisi kama Wizara tunapongeza uwekezaji huu utakaosaidia kupanua sekta
ya kuku nchini, utachechemua biashara na kuongeza mzunguko wa fedha, hivyo
tunamshukuru Rais Samia kwa kuweka
mazingira mazuri ya uwekezaji hapa
nchini na matokeo yake tunayaona," alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa kuku watakaozalishwa katika shamba hilo watauzwa maeneo mbalimbali hapa nchini pamoja
na nje ya nchi hali itakayopelekea ongezeko la kipato kwa mtu mmoja moja na
taifa kwa ujumla.
Aidha aliwataka wananchi wa Wilaya ya
Siha kuwakumbatia wawekezaji wa shamba hilo lengo likiwa ni kunufaika na
ufugaji huo ikiwa ni pamoja na kuuza vifaranga hao kwa nchi za jirani.
" Tumekuwa tukiagiza vifaranga wazazi kutoka nje na kutumia fedha
nyingi, uwepo wa mradi huu utapunguza matumizi ya fedha za kigeni na kukuza
uchumi wa nchi kwa kuwa tutakuwa tunazalisha
hapa hapa nchi, aliongeza.
Pia, alifafanua kuwa uwepo wa wawekezaji hao utasaidia kutekeleza adhma ya
serikali ya kutengeneza ajira zaidi
ya milioni 8 ifikapo 2025 pamoja na
kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja.
Akielezea mradi huo Mwenyekiti wa Kampuni ya Aviagen Afrika Mashariki Bw.
Kester lyaruu alisema kuwepo kwa mradi huo kutachangia kuleta usalama wa
chakula pamoja na kuzuia uingizwaji wa vifaranga visivyo salama kutoka nje ya
nchi.
"Mradi huu utasaidia uchumi wa nchi na kuongeza lishe kwa wananchi wa
kawaida ambao wataweza kupata vifaranga hao kwa bei nafuu" alisema Lyaruu.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Thomas Apson alisema mradi huo wa kuku ni
wa kuzalisha vifaranga wazazi mababu na mabibi watakaoendelea kuzalisha kuku
wengi zaidi.
Mwananchi kutoka Wilaya ya Siha Bi. Witness Philemon alisema, wanapata ajira mbalimbali kutokana na uwekezaji huo na kuiomba Serikali kuanzisha miradi ya ufugaji kuku katika vijiji na vitongoji Ili kusaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment