SERIKALI imedhamiria kuhakikisha makundi yote katika jamii yanashiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa Mipango, Sera na Miongozo inayotegenezwa ili kila mmoja anufaike na fursa zilizopo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju alipokuwa akifungua kikao cha wadau wanaopitia na kutoa maoni juu ya kitini cha mwongozo mafunzo ya uwiano wa kijinsia na ushirikishwaji wa Jamii, kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 01, 2022.
Mpanju amesema kitini hicho kitatumika kuhakikisha kwenye huduma zote zinazotolewa nchini zinazingatia uwiano na usawa wa kijinsia na ujumuishaji wa jamii kwa ujumla kwa misingi ya wenye mahitaji maalum.
"Kwa kawaida unapotaka kuongelea Maendeleo na Ustawi lazima uyape mahitaji yake jicho la kipekee ili Maafisa Ustawi na Maafisa Maendeleo ya Jamii wanapotoa huduma kwa jamii wazingatie upekee kwa Makundi hayo.
No comments:
Post a Comment