MADEREVA WA MALORI NA MABASI WAMUANGUKIA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI MIKATABA YAO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 24 September 2022

MADEREVA WA MALORI NA MABASI WAMUANGUKIA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI MIKATABA YAO

 

Mwenyekiti  wa Chama cha Madereva  Hassan Dede akiwa ameongozana na Madereva wenzake katika harakati za kudai haki zao.

Na Dunstan Mhilu

CHAMA Cha Madereva wa Malori na Mabasi ya Masafa marefu Tanzaniania kimemuangukia Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la mikataba yao ya ajira dhidi yao na waajiri wao.

Wakitoa kilio Chao mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Dede alisema wanaamini serikali inayoongozwa na Rais Samia ni sikivu na kwakupitia vyombo vya Habari atapata taarifa hii na atafanya jambo.

“Tunaimani kubwa sana na Rais wetu kwa mamlaka aliyonayo atafanya jambo, kwakuwa madereva nao ni wanataaluma kama wanataaluma wengine ambao wana stahili kupata stahiki zote kama wengineo waliopo katika sekta binafsi wanavyothaminiwa na waajiri wao.

Dede alisema haiyumkiniki mwajiri ana mkabidhi gari dereva yenye thamani ya Sh 400 milioni na mzigo wenye thamani ya Sh 100 milioni apeleke nchini DRC au Malawi halafu dereva huyo anaambulia Sh 100,000 kwa mwezi na Posho ya Sh 300,000 awapo safarini ambapo hukumbana na changamoto mbalimbali.

Dede alisema madereva ni watu muhimu na injini kwa uchumi wan chi yeyote ile kwakuwa kila sekta nchini inawategemea madereva

“Unapozungumzia Bandari kuwa ni lango kuu la uchumi huwezi iendesha Bandari pasipo mchango wa madereva ambao husafirisha mizgo au bidhaa kutoka Bandarini na kuisafirisha kwenda mataifa ya jirani hivyo basi serikali kwakuwa ina mkono mrefu na haishindwi basi iharakishe suala hilo ambalo limepigiwe yowe muda mrefu lakini hakuna kilichofanyika”alisema Dede

Aidha Dede ameiomba serikali kupunguza utitiri wa kodi uliopo katika sekta ya usafiri nchini ili waajiri waweze kuwalipa mishahara minono kuliko ilivyosasa ambapo waajiri wengi husingizia tozo nyingi wanazotozwa na serikali kuwa ndiyo chanzo cha kutolipwa vizuri.

Kwa upande wake John Pazia anayefanya kazi katika moja ya malori yaendayo nchi jirani amelalamikia kwa baadhi ya watunga sheria kuwa wafanyabiashara na ndiyo maana suala lao halizingatiwi.
“Wanasiasa baadhi waliopo Bungeni ni wamiliki wa malori na mabasi ndiyo maana suala hili halipewi uzito yani kufanikiwa kwa hili suala ni Mkuu wa Nchi tu Mama yet una Rais wetu kipenzi kulifanyia kazi mchakato ulianza 2015 lakini hadi leo bado tunasotea”alisema Pazia

Vilevile madereva hao wameonesha umuhimu wa wao kupatiwa mikataba na kuunganishwa na huduma za bima pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo serikali na madereva watanufaika na michango ya bima ya afya watakayokatwa na michango yao kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Julai 26, 2022 alikutana na Mawaziri akiwemoWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,  Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako na kuendesha kikao kwa ajili ya kutatua changamoto za madereva kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha inaendelea kusimamia madai ya madereva pamoja na haki za waajiri katika kutekeleza madai ya madereva wa malori.

 “Lengo ni kuhakikisha madereva wanaendelea na ajira zao na wanapata maslahi yao kwa mujibu wa sheria ili waweze kuendesha shughuli zao na familia zao na Serikali itasimamia madai yao na haki za waajiri katika kutekeleza madai ya madereva wasije wakawajibika na vitu ambavyo haviko kwenye sheria zetu za nchi.”

 Majaliwa ametumia fursa hiyo kukitaka Chama Cha Madereva nchini kiruhusu huduma za usafirishaji ziendelee kutolewa wakati Serikali ikiendelea kushughulikia masuala yao.

“Serikali haitaridhika kuona madereva wanalalamika kila siku na pia si vizuri waajiri wakabebeshwa mizigo iliyo nje ya sheria. 

No comments:

Post a Comment