KUFANYIKA KWA VIKAO VYA UONGOZI CHAMA CHA MAPINDUZI NGAZI YA TAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 25 September 2022

KUFANYIKA KWA VIKAO VYA UONGOZI CHAMA CHA MAPINDUZI NGAZI YA TAIFA


KUFANYIKA KWA VIKAO VYA UONGOZI CHAMA CHA MAPINDUZI NGAZI YA TAIFA.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwataarifu wanachama wake na watanzania wote kuhusu kufanyika kwa vikao vya kawaida vya uongozi ngazi ya Taifa Jijini Dodoma kuanzia tarehe 26 Septemba, 2022 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) na tarehe 27 na 28 Septemba, 2022 Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC).

Pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama ambao wameomba uongozi katika ngazi ya wilaya.

Vikao hivyo vilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kilichofanyika tarehe 22 na 23 Septemba, 2022 Jijini Dodoma.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI NA UENEZI.
25 Septemba, 2022.

No comments:

Post a Comment