KIOO LTD YAIKADHI MASHINE YA KUCHAPISHA MITIHANI SEKONDARI YA VIANZI, MKURANGA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 23 September 2022

KIOO LTD YAIKADHI MASHINE YA KUCHAPISHA MITIHANI SEKONDARI YA VIANZI, MKURANGA

Meneja Uhusiano wa Kioo Ltd, Richard Stoni Msimule  akimkabidhi Mashine ya kuchapishia mitihani na nyaraka za osifi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Vianzi mkoani Pwani hivi karibuni.

Na Dunstan Mhilu, Mkuranga

KAMPUNI ya Kioo Ltd imeikadhi mashine ya kuchapisha mitihani na shughuli za kiofisi shule ya sekondari Vianzi iliyopo Mkuranga Mkoani Pwani yenye thamani ya Sh 2,900,000.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Richard Msumule alisema wamewiwa kutoa msaada wa mashine hiyo kwa shule ya sekondari vianzi kwa kuwa walikuwa na uhitaji wa kifaa hicho.

“Katika Kampuni yetu tunao utaratibu wa kusaidia miradi na huduma mbalimbali kutokana na uhitaji uliopo, leo tumetoa mashine hii kwakuwa Shule ya sekondari Vianzi haina mashine ya kuchapishia mitihani na shughuli za kiofisi ndiyo maana tumeona tuchangie katika uhitaji huo”alisema Richard.

Richard aliongeza kuwa mashine hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa shule hiyo kwakuwa ina idadi kubwa ya wanafunzi wasiopungua 6000 ambapo walikuwa wakitumia gharama kubwa kwakuchapisha mitihani yao nje ya shule.

Kwa upande Kaimu Meneja rasilimali watu , Kapil Dave alisema wameamua kuipatia mashine hiyo kwakuwa vianzi ni eneo lao la kimkakati ambapo huchimba mchanga kwa ajili ya matumizi yao ya uzalishaji chupa za kioo kwa ajili ya Kampuni mbalimbali.

“Vianzi ndipo tunapochimba mchanga hivyo tumeona ni vyema tuwashike mkono ndugu zetu hawa ili kuwapunguzia gharama za uendeshaji pamoja na kuokoa mud ana usiri kwakuwa mitihani ni siri hapaswi kuchapishwa kiholela”alisema

Dave ameongeza kuwa wametekeleza miradi mbalimbali katika eneo hilo ambapo kwa sasa wanashiriki ujenzi wa Daraja linalounganisha Vianzi na Mkuranga ambapo wao wamechangia karavati kwa ajili ya ujenzi huo.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Veronika Temu aliushukuru uongozi wa Kampuni hiyo na kusema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka.

“Tunaishuku Kampuni ya Kioo kwakutusaidia mashine hii ambayo imekuja wakati muafaka tunaomba iendelee kutushika mkono katika mahitaji mengine pale tutakapobisha hodi katika ofisi zao wasituchoke,” alisema Veronica.

Kwa upande wake Mwalimu wa Hisabati na Fizikia katika shule hiyo Adam Banda alisema mashine hiyo itawaongezea ufanisi na kudhibiti uvujaji wa mitihani.

“Kwetu sisi ni msaada mkubwa sana nyaraka za ofisi ni siri ya ofisi fulani inapofikia hatua nyaraka za ofisi kuchapwa maeneo yasiyo rasmi ni jambo la hatari lakini tunashukuru Kioo Ltd wametushika mkono tutaituza na itatufaa,” alisema Banda.

No comments:

Post a Comment