BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 August 2022

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akipata maelezo kuhusu huduma za uwezeshaji sekta ya kilimo zinazotolewa na Benki ya CRDB kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa Benki ya CRDB, Maregesi Shaaban (kulia), wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya. Katikati ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za juu kusini, Jeniffer Tondi akati akimpatia maelezo kuhusu huduma za uwezeshaji sekta ya kilimo zinazotolewa na Benki ya CRDB, wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya. Katikati ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Benki ya CRDB wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
======= ======= =======

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Philip Mpango ameitaka Benki ya CRDB kupitia Umoja wa Mabenki Tanzania kutoa Elimu ya namna inavyotoa mikopo kwa wakulima ili waweze kuwa na uthubutu na kuleta tija kwenye uzalishaji nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane 2022 kitaifa yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
"Nachukua fursa hii kutaka Benki ya CRDB kupitia Umoja wa Mabenki Tanzania kutoa Elimu ya namna bora ya kutoa mikopo kwa wakulima ili waweze kuwa na uthubutu na kuleta tija kwenye uzalishaji nchini" alisema Dkt. Mpango.

Pia ametoa wito kwa vyama vyote vya ushirika nchini kujiunga na Benki ya CRDB ili viweze kujikwamua kiuchumi na kupata mazingira wezeshi katika sekta zote za kiuchumi.
Akielezea mchango wa Benki ya CRDB katika sekta ya kilimo nchini, Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban alisema “Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Benki ya CRDB imetoa jumla ya mikopo ya kilimo inayofikia TZS. 769 Bilioni, sawa na asilimia 43% ya mikopo yote ya kilimo inayotolewa na mabenki hapa nchini.

Kati ya mikopo hiyo, TZS. 494 Bilioni imeelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati hivyo kusaidia zaidi ya AMCOS 472 kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo (mikopo ya pembejeo, maghala, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao, mikopo kwa ajili ya miradi ya ufugaji, uwekezaji kwenye misitu na mazao yake pia uwekezaji kwenye uvuvi). Kwa kipindi cha miaka mitano ilyopita hadi kufikia mwezi Juni 2022, Benki ya CRDB imetoa mikopo kwenye sekta ya kilimo inayofikia kiasi cha TZS. 2.6 Trilioni”.

Benki ya CRDB ndio Benki pekee ya biashara iliyoanza kutoa mikopo nafuu zaidi kwenye sekta ya kilimo kwa riba ya asilimia tisa (9%) tu kwa mwaka. Hali hii imechagiza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na hivyo kukuza uchumi wa nchi kupitia ajira na pato la taifa kwa ujumla.

Wakulima wadogo wadogo kupitia kwenye vyama vya Ushirika wanaunganishwa na mifumo madhubuti ya kifedha kupitia mtandao imara wa Benki ya CRDB. Mkulima anaweza kupata huduma za kifedha kupitia CRDB Wakala, simu za mkononi hivyo kujijengea tabia za kujiwekea akiba kupitia huduma rahisi zinazopatikana hadi vijijini.

Naye Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jeniffer Tondi alimweleza Makamu wa Rais kuwa Benki ya CRDB iko tayari kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa sekta ya kilimo katika kuuimarisha ushirika. Tondi alisema Benki ya CRDB mpaka sasa imehusika katika kuzijengea uwezo benki mbili za ushirika ambapo TZS. 3.2 Bilioni zilitolewa kwa TACOBA na TZS. 7.0 Bilioni kwa KCBL, hivyo kuwezesha Benki hizi za Ushirika kupata mtaji unaofikia kiasi cha TZS. 10.2 Bilioni

No comments:

Post a Comment