SHULE YA SEKONDARI TUMAINI YAJIWEKEA LENGO KUWA MIONGONI MWA SHULE 30 BORA KITAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 24 July 2022

SHULE YA SEKONDARI TUMAINI YAJIWEKEA LENGO KUWA MIONGONI MWA SHULE 30 BORA KITAIFA

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Tumaini kwenye hafla ya Siku ya Kitaaluma ya shule hiyo iliyofanyika jana ambapo wanafunzi na walimu waliofanya vizuri kwenye masomo walipewa zawadi mbalimbali zikiwamo fedha taslimu. Kushoto kwake ni Mkuu wa shule hiyo, Zainabu Mtinda.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda  akihutubia kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Zainabu Mtinda na Kulia ni Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Iramba, Patricia Michael ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora na Afisa Elimu Sekondari wa wilaya hiyo.

Mkuu wa shule hiyo, Zainabu Mtinda akizungumza kwenye hafla hiyo.

Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Iramba, Patricia Michael akizungumza kwenye hafla hiyo ambapoalitumia nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuandaa siku hiyo muhimu ya kitaaluma.
Mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, Beatrice Nalingigwa akizungumza kwenye hafla hiyo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinampanda, Elias Wilfred akizungumza kwenye hafla hiyo.

Afisa Elimu Kata ya Kinampanda, Mathayo Lengael Kaaya akizungumzia umuhimu wa siku hiyo ya taaluma na kueleza kuwa inawafanya wanafunzi, walimu na wafanyakazi wa kada nyingine kuwa na mori wa kufanya kazi baada ya kupatiwa tuzo mbalimbali.

Wanafunzi wakitoa maelezo kuhusu matumizi ya lugha ya kiingereza  kwa mkuu wa wilaya hiyo.

Mwanafunzi wa shule hiyo, Manka Munisi wa kidato cha tatu akitoa ya matumizi ya maneno ya lugha  kiingereza kwa mkuu wa wilaya.

Mkuu wa Wilaya hiyo Suleiman Mwenda akiwasikiliza wanafunzi walivyokuwa wakielezea jinsi volkano inavyotokea katika milima.

Wanafunzi wakiwa tayari kutoa maelezo ya jinsi volkano inavyokuwa katika milima.

Wanafunzi wa shule hiyo wakimsubiri mkuu wa wilaya ili waweze kuzungumzia namna ya kuandaa chakula. Kutoka kushoto Yousrath Hamisi, Selina Mziba na Michelle Singla.

Wanafunzi wa shule hiyo wakimsubiri mkuu wa wilaya ili wazungumzie uandaaji bora wa mboga za majani kabla ya kuzipika. Kutoka kushoto ni Neema Jackson, Sabina Charles na Leah Isack.

Wanafunzi wa shule hiyo,  kutoka kushoto Yousrath Hamisi, Selina Mziba na Michelle Singla wakijadiliana wakati  wakimsubiri mkuu wa wilaya ili waweze kuzungumzia namna ya kuandaa chakula.

Mwanafunzi wa shule hiyo,  Yousrath Hamisi (kushoto) akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya namna bora ya kuandaa chakula.

Mwanafunzi Neema Jackson (kushoto) akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya namna bora ya kuandaa mboga za majani.


Wanafunzi wakielezea namna bora ya kuandaa majisafi na salama.

Wanafunzi wakielezea namna ya matumizi ya ATM Mashine.

Wanafunzi wa Sekondari ya Lulumba iliyopo wilayani humo walikuwa ni sehemu ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo hapo wanaonesha furaha zao za kushiriki tukio hilo.

Taswira ya hafla hiyo.

Wanafunzi wakiimba wimbo maalum unaohusu siki hiyo ya taaluma.

Walimu wa shule hiyo wakionesha furaha yao katika hafla.

Walimu wakionesha umahiri wa kucheza Kwaito kwenye hafla hiyo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakiwa kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi akitoa zawadi kwa walimu.

Zawadi zikitolewa.

Mmoja wa wafanyakazi wa shule hiyo akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kupokea zawadi.

Mkuu wa wilaya akimfunga mkanda wa pongezi mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri.

Wanafunzi waliofanya vizuri wakiwa na mikanda yao ya kupongezwa.

Wanafunzi wakiigiza igizola kuhamasisha sensa ya watu na makazi na uadilifu kwa wasimamizi na makarani wa sensa hiyo.

Mkuu wa shule hiyo Zainabu Mtinda (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyotolewa na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo. 

Na Doto Mwaibale, Iramba 

SHULE ya Sekondari ya Tumaini inayomilikiwa na Serikali iliyopo Kata ya Kinampanda wilayani Iramba mkoani Singida imejiwekea lengo la kuwa miongoni mwa shule 30 bora kitaifa kwa kidato cha tano na sita na ya 50 kwa kidato cha kwanza hadi Nne.

Mkuu wa Shule hiyo, Zainabu Mtinda, alisema hayo jana kwenye hafla ya siku ya kitaaluma ya shule hiyo ambapo wanafunzi na walimu waliofanya vizuri kwenye masomo walipewa zawadi mbalimbali zikiwamo fedha taslimu vyeti.

"Ipo mikakati ya ndani, ya kiwilaya,mkoa na kitaifa ambapo mkakati mmoja wapo ni kufanya vizuri iwe katika 30 bora kwa matokeo ya kidato cha Tano na Sita, na iwe ya miongoni mwa shule 50 bora kitaifa kwa kidato cha Kwanza hadi cha Nne," alisema.

Alisema malengo hayo yatatimia kwani kila mwaka matokeo ya shule hiyo yanekuwa yakipanda ambapo kuanzia mwaka 2020 hadi 2022 hakuna wanafunzi waliopata daraja la Nne na sifuri kwa matokeo ya kidato cha Sita.

Mtinda alisema kwa matokeo ya kidato cha Nne, mwaka 2020 Shule Sekondari Tumaini ilishika nafasi ya sita kimkoa kati ya shule 164 na mwaka jana 2021 ilishika nafasi tano kimkoa na kupata GPS nzuri ambayo ni 2.4240.

Aidha, Mkuu huyo wa shule alisema pamoja na mafanikio yote hayo bado kuna changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kusomea wanafunzi walemavu wa macho na pia shule kutokuwa na uzio kwa ajili ulinzi na usalama kwa wanafunzi..

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kuiboresha shule hiyo ili kuwa na mazingira mazuri kwa wanafunzi kujifunza.

Mwenda alisema mfano katika mwaka wa fedha uliopita wa 2021/2022 shule hiyo imepatiwa zaidi ya Sh.bilioni 1.7 kwa ajili ya kujenga mabweni,madarasa na kuyaboresha madarasa yaliyopo.

Alisema nayo Benki ya NMB katika kuunga juhudi za serikali imetoa vitanda 40 vya kulala wanafunzi 80 wa shule ya sekondari Tumaini ambayo kila mwaka imekuwa ikifanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha pili, nne na sita na hivyo kuibeba wilaya na mkoa wa Singida.

Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali katika kugharamia elimu bure Wilaya ya Iramba inapewa Sh.milioni 654 kwa shule za sekondari na Sh.millioni 403 kwa shule za msingi.


No comments:

Post a Comment