Camilius Wambura |
RAIS Samia Suluhu
Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura kuwa Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP), anayechukua nafasi ya
Simon Sirro.
Taarifa kutoka ikulu
inasema;-
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022
amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
Amempandisha cheo
Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Amemteua aliyekuwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Zimbabwe.
Amempangia kituo
Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Zambia.
Amemteua Dkt. Suleiman
Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Uteuzi huu umeanza
tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00
Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.
Wakati huo huo, Mhe.
Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: -
Amemteua Kamishna wa
Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki.
Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.
Amemteua Kamishna wa
Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua
nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.
Amemteua Kamishna wa
Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;
Amempandisha Cheo Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi
Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu
mengine.
Amempandisha Cheo
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
No comments:
Post a Comment