Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
ALIYEKUWA Mgombea ubunge jimbo la
Nungwi Zanzibar kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Hussein Ramadhan Layya
maarufu Masokolo amejitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Msokolo akizungumza na waandishi wa habari alisema amechukua uamuzi huo
baada ya kutafakari mwenendo wa chama chake ambao hautowi mwelekeo wa
kukiimarisha chama kuanzia ngazi za chini.
Alisema wakati yupo katika Chama cha Demokrasia Makini dhamira yake kubwa ilikuwa ni kuisadia jamii
na kikiimarisha kwa kutatua kero mbalimbali.
Msokolo amesema mfumo wa kisiasa ulivyo sasa nchini unaifanya CCM kuwa na
tofauti kubwa na vyama vingine vya siasa na ndio maana kimekuwa kikipata
matokeo mazuri kila uchaguzi mkuu unapofanyika.
Alieleza kushangazwa kuona kwamba ndani ya Chama cha Demokrasia Makini
tangu umalizike uchaguzi mkuu wa 2020 hakijawahi kukaa kufanya tathimini kama
ambavyo CCM imekuwa ikifanya ili kubaini ni wapi walikosea hadi wasipate
matokeo mazuri.
Aidha, Msokolo alizindua tawi katika
jimbo la Nungwi ikiwa ni historia ya chama hicho kuasisi tawi eneo lenye
upinzani mkubwa ambapo aliweza kuvuna kundi kubwa la vijana wazee na kinamama
kujiunga na chama hicho.
"Pamoja na kazi kubwa niliyoifanya kukiimarisha chama nilipoona sipewi
ushirikiano nikaona ni nafasi yangu ya
kurudi ccm ambapo anaamini kwamba kuna ushirikishwaji mzuri katika ngazi
zote kuanzia shina,tawi,wadi,jimbo wilaya,mkoa,hadi taifa," alisema
Msokolo.
Msokolo kurudi CCM kuna tija gani,ni mtu mwenye kundi kubwa la watu
wanaoamini kwamba anao uwezo mkubwa wa kuwasaidia na kuisaidia jamii kwa
ujumla.
Msokolo pia ni mtu aliyejifunza mengi katika nchi mbalimbali na mwenye
vipaji tafauti,kama vile sanaa ya uigizaji,uchoraji,uandishi wa
habari,dereva,fundi seremala,mtunza ubora,msimamizi wa manunuzi,mtunza stoo na
meneja usafirishaji.
Kama CCM wakimtumia ipasavyo
watakuwa wamelamba karata yenye thamani,na isitoshe katika kipindi hiki
alichorudi ni wakati muafaka wa kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote katika
chama kwani anao uwezo mkubwa na ni mbobezi katika laaluma tofauti na medani ya
siasa.
No comments:
Post a Comment