DK. MWIGULU: UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ILINGANE NA THAMANI YA FEDHA ZINAZOTOLEWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 28 July 2022

DK. MWIGULU: UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ILINGANE NA THAMANI YA FEDHA ZINAZOTOLEWA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi, akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa, kilichofanyika leo Julai 27, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ambaye alikuwa Mwenyekiti akiongoza kikao hicho.

Makamu Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mbunge wa Singida, Kaskazini, Ramadhan Ighondo akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimba akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliwapongeza wabunge wa mkoa huo kwa kazi nzuri wanayifanya.

Wabunge wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

kikao kikiendelea.
Wakuu wa idara mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.


Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Mutahibirwa akijitambulisha kwenye kikao hicho.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege akijitambulishakwenye kikao hicho.

Taswira ya kikao hicho.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya katibu Tawala wa Mkoa.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea. Kushoto ni Mwakilishi wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Aysharose, Mariama Ntembo na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Haika Massawe wakiwa kwenye kikao hicho.

Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk. Pius Chaya akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Eliya Digha akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega  akichangia jambo kwenye kikao hicho wakati akiomba kujengewa barabara.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza kwenye kikao hicho.

Meneja  wa  Tanroads, Mkoa wa Singida Mhandisi Msama K. Msama akizungumzia matengenezo ya barabara mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Jumanne Mlagaza akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye kikao hicho.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu akizungumza kwenye kikao hicho. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi amesema miradi yote ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa nchini ilingane na thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali.

Dk.Mwigulu ameyasema hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa, kilichofanyika leo Julai 27, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hii ili kumuheshimisha nawaombeni miradi hiyo mnayoisimamia kuijenga ilingane na thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali” alisema Dk.Mwigulu.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho  aliwaagiza Wakala wa Barabara Vijiini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) mkoani hapa kuhakikisha fedha zilizotengwa na serikali zinatumika kuleta mabadiliko makubwa kwenye miundombinu ya barabara.

Alisema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo na ufunguzi wa barabara mpya ili ziweze kusaidia kuleta maendeleo ya wananchi.

"TARURA na TANROAD mhakikishe fedha zinatumika vizuri kukarabati na kuanzisha barabara mpya katika maeneo yenye changamoto za upitaji ili kukamilisha kauli ya 'Tunawafikisha Pasipo Fikika' inatimia," alisema.

Dk.Mahenge alisema bado yapo maeneo mengi katika mkoa huu ambayo yana changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara hivyo ajenda hiyo ni muhimu kujadiliwa kwa kina kwa kuwa ni chombo cha kuleta maendeleo ya wananchi.

Aidha, aliwagiza mameneja  wa barabara zote mkoani hapa wahakikishe wanaongeza usimamizi wa wakandarasi  ambao wanapewa zabuni mbalimbali za ujenzi wakati hawana uwezo wa kutosha jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi.

"Mfano katika Wilaya ya Manyoni pale kuna mkandarasi alipewa fedha za kujenga barabara ya Majengo- Hospitali ya Wilaya  lakini mpaka sasa haijakamilika na kusababisha malalamiko ya wananchi," alisema.

Dk. Mahenge alitumia nafasi hiyo kuwaomba TANROADS na TARURA kutenga maeneo katika barabara kwa ajili ya kupitisha mifugo ili kuzitunza na akasisitiza elimu itolewe kwa wananchi ya utunzaji wa barabara hizo.

Aidha, Mahenge aliwapongeza wabunge wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano wao katika kuwaletea maendeleo na kupambania upatikanaji wa fedha za barabara kwa kiasi kikubwa.

 Mbunge wa Singida Mashariki, Jumanne Mtaturu alisema pamoja na jitihada za kutengeneza na kufungua barabara mpya lakini kasi ya uharibifu wa barabara hizo imekuwa ikiongezeka sana.

Kutokana na hali hiyo, Mtaturu amewataka wataalamu kuangalia chanzo cha tatizo ikiwemo upitishaji wa mifugo kwenye barabara na matumizi ya mabasi madogo 'Noah' kwa kuwa imeonekana sehemu mbalimbali wanakotumia usafiri wa aina hiyo barabara zinaharibika zaidi.

Mtaturu aliomba kuwepo kwa taa za barabarani katika miji midogo ikiwamo Ikungi na maeneo mengine ili kuweza kuchangamsha mji jambo ambalo meneja wa TANROAD na TARURA wamelipokea na kuahidi kulifanyia kazi.

Awali akitoa taarifa, Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida,  Mhandisi Tembo David alisema mkoa una mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 5,666.412.

Mhandisi Tembo alisema barabara zenye urefu wa kilometa 1360.6 sawa na asilimia 24 zina hali nzuri na zinapitika majira yote ya mwaka wakati na za kilometa 1700.8 sawa na asilimia 30 zina hali ya wastani  na  kilometa 2607.9 sawa na asilimia 46 zina hali mbaya  na hupitika majira ya kiangazi tu.

Meneja  wa  Tanroad, Mhandisi Msama Kosani Msama alisema katika mpango wa bajeti wa mwaka 2022/23 Mkoa wa Singida wameweka mpango wa kuweka taa za barabarani katika maeneo mbalimbali.

 Alitaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni katika barabara inayoanzia  ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hadi  Mwenge katika barabara ya Singida – Gehandu na kuanzia Skyway hadi Kona ya Mohamedi, Njuki hadi Mizani katika barabara ya Dodoma – Singida – Mwanza.

Alisema Tanroad inaendelea kuimarisha  barabara kuu ya lami Dodoma – Singida – Mwanza kwa kufanya matengenezo mbalimbali na ujenzi wa daraja eneo la Kyengege na kuimarisha barabara kuu ya Rungwa (Mbeya/Singida Mpakani) – Itigi – Mkiwa.

Mhandisi Msama ametoa wito kwa watumiaji wengine  kuomba kibali endapo wanataka kutumia barabara kwani tatizo la upitishaji wa mifugo imekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa barabara.

Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wabunge na wenyeviti wa halmashauri za wilaya mkoani hapa kila mmoja aliomba barabara zilizoombwa kujengwa zijengwe kwa wakati akiwepo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega ambaye alitaka wilaya hiyo ipewe kipaaumbele kwa kuzingatia kuwa haina barabara ya kiwango cha lami inayounganisha wilaya hiyo na makao makuu ya wilaya ukilinganisha na halmashauri zingine.

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu akizungumza kwenye kikao hicho alisema miradi hiyo inafanywa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo alimshukuru Mwenyekiti wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kuitekeleza. 

 

No comments:

Post a Comment