MAWAZIRI WANAOSIMAMIA UCHUKUZI WA TANZANIA, DRC NA BURUNDI WASAINI RIPOTI YA WATAALAM YA MRADI WA SGR MJINI KINSHASA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 13 June 2022

MAWAZIRI WANAOSIMAMIA UCHUKUZI WA TANZANIA, DRC NA BURUNDI WASAINI RIPOTI YA WATAALAM YA MRADI WA SGR MJINI KINSHASA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (kulia) akiwa na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa DRC Congo Cherubi Senga (katikati) na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa Burundi, Marie Nijimbe (kushoto)wakionyesha  taarifa ya watalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye Jumla ya Kilomita 939, uliofanyika mjini Kinshasa mara baada ya Mawaziri hao kuisaini mjini Kinshasa.

 

Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kushoto) akiwa na Makatibu wa Wizara zinazosimamia Uchukuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi wakisaini ripoti ya Wataalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumburaa-Uvinza-Kindu wenye jumla ya Kilomita 939, mjini Kinshasa.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika mkutano uliwakutanisha Mawaziri wanaosimamia Uchukuzi wa Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Makatibu Wakuu na Wataalam wa nchi hizo (hawapo pichani) kujadili na kusaini ripoti ya Wataalam ya Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Uvinza-Musongati-Gitega-Bujumbura-Uvinza-Kindu wenye Jumla ya Kilomita 939, mjini Kinshasa.

No comments:

Post a Comment