BANDARI YA KAREMA KUKABIDHIWA MWEZI JULAI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 7 June 2022

BANDARI YA KAREMA KUKABIDHIWA MWEZI JULAI

 

Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika, Manga Gassaya, akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kulia) kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa gati katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea ujenzi wake Mkoani humo. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Usafiri Majini- Sekta ya Uchukuzi, Mussa Shashula.


Muonekano wa gati jipya katika bandari ya Karema Mkoani Katavi, kukamilika kwa gati hiyo kutaruhusu meli zenye urefu wa mita 150 na upana wa mita 15. Mradi wa upanuzi wa bandari hiyo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya Jengo la Abiria katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi. Mradi wa bandari hiyo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa sasa umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Interconsult ltd, Elisante Urassa akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kulia), kuhusu hatua iliyofikiwa ya eneo la kuwekea mizigo katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea ujenzi wake.


Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi akizungumza na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mpanda, Jeff Shantiwa, baada ya kuwasili Mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi.

No comments:

Post a Comment