WAZIRI MBARAWA ARUHUSU MAGARI KUPITA JUU BARABARA YA CHAN'GOMBE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 30 May 2022

WAZIRI MBARAWA ARUHUSU MAGARI KUPITA JUU BARABARA YA CHAN'GOMBE

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuruhusu kuanza kutumika kwa njia moja katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila (katikati), alipokagua na kuruhusu kuanza kutumika kwa njia moja katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kabla ya kuruhusiwa kwa magari kuanza kupita katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo.

Taswira ya magari yakipita njia moja katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.

Gari la Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, pamoja na la Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila yakipita kuashiria kuanza kutumika kwa njia moja katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo ameruhusu kuanza kutumika kwa njia moja ya barabara ya Juu Chang'ombe ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kuanza kutumika kwa barabara hiyo, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kuhakikisha magari yanayotumia njia hiyo kwa sasa yanazingatia sheria za mwendo kwani bado ujenzi unaendelea eneo hilo.

Alisema kutumika kwa barabara hiyo kutasaidia kupunguza msongamano hivyo, kuwasaidia watumiaji  wa barabara hiyo wapate muda wa kutosha kufanya shughuli zao kwani msongamano  katika eneo hilo unawapotezea muda.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mativila amemhakikishia  Mhe. Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka BRT2 utakamilika kwa ubora na kwa wakati.

Eng. Mativila  amesema  ujenzi wote wa Barabara za Juu za Chang'ombe na Chuo cha Uhasibu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu. 

 Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasilino Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

No comments:

Post a Comment