Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa MACHINGA Iringa, shirika la Kijana Amka Sasa Organization (KASO), chuo cha CDTI, mkurugenzi wa Envibright group Paul Myovelah, diwani wa kata ya Makorongoni N. K wakati wa siku ya kufanya usafi.
Mkurugenzi wa Envibright Group, Paul Myovelah akiongea na wananchi, wadau, MACHINGA na wanafunzi wa chuo cha RUAHA CDTI juu ya umuhimu wa kutunza mazingira.
Mkufunzi wa chuo cha RUAHA CDTI Muhidin Galiatano akiwa ameongozana na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliojitokeza kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa
WANANCHI wa Mkoa wa Iringa wametakiwa kufanya usafi kila wakati kwa ajili ya kuyatunza na kulinda mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na magonjwa ya milipuko na yanayotokana na madhara ya mazingira kuwa machafu.
Akizungumza wakati wa kufanya usafi mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Kijana Amka Sasa Organization lililopo mkoani Iringa, Baby Baraka Chuma alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa na utamadumi wa kufanya usafi kila wakati.
Chuma alisema kuwa wameamua kufanya usafi katika mji wa Manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwaonyesha vijna namna kutunza mazingira yanayowazunguka kwa ajili ya kulinda afya zao.
Alisema kuwa shirika hilo la Kijana Amka Sasa Organization (KASO) limeshiriki katika siku ya kufanya usafi kwa lengo la kuwaeleza vijana kuishi na utamaduni wa kufanya usafi na kutunza mazingira kila wakati kwa faida ya afya za wananchi wa taifa hili na nje ya taifa la Tanzania.
Chuma alisema kuwa kufanya usafi na kuishi katika mazingira yaliyo salama yanachangia kwa kiasi kikubwa vijana kutimiza ndoto zao kwa kuwa kunawafanya vijana waishi maisha yasiyo na magonjwa ya milipuko.
mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Kijana Amka Sasa Organization lililopo mkoani Iringa, Baby Baraka Chuma alimazia kwa kuwaomba wananchi wa Iringa kuyatunza mazingira kama ambavyo wamefanya wao kwa kushirikiana chuo cha maendeleo ya jamii Iringa CDTI na Serikali ya Manispaa ya Iringa kufanya usafi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Envibright group Paul Myovelah alisema kuwa kufanya usafi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa umekuwa umaduni ambayo unafanywa kama sherehe ya kila siku.
Myovelah alisema kuwa Iringa inatakiwa kuelendeleza umoja walionao katika kufanya usafi kama utamadumi wao wa kila wakati wawapo nyumbani, kazini na kwenye shughuli zote za kila siku.
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kudumisha utamadumi wa kufanya usafi kila wakati pale panapohitajika.
Myovelah alisema kuwa ni wakati wa taasisi,mashirika, makampuni na wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya utunzaji na ufanyaji wa usafi wa mazingira kila siku wanapopata nafasi hiyo.
Alimazia kwa kusema kuwa Iringa kufanya usafi ni sherehe ya kila siku na ndio utamadumi wa wananchi karibia wote.
Naye mkufunzi wa chuo cha RUAHA CDTI Muhidin Galiatano alisema kuwa Wanafunzi wameshirikishwa kwa kuwa wao ni viongozi wa baadae kutokana na elimu ya maendeleo ya jamii wanayoisomea chuoni hapo.
Galiatano alisema kuwa wamewashirikisha Wanafunzi kwa kuwa wamekuwa wanafundishwa kufanya usafi kila siku kutokana maisha wayoyaishi wawapo chuoni hapo.
Alisema kuwa zaidi ya watu elfu moja wameshiriki kufanya usafi kuzunguka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Iringa
Galiatano alisema kuwa Iringa ni mmoja ya mikoa ambayo inaongoza kwa kufanya usafi na ndio jadi ya wanairinga hivyo kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi ni Jambo la kukumbushana.
Katika kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada ambaye alisema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kufanya usafi kila wakati ili kufanya biashara kwenye mazingira mazuri.
Ngwada alisema kuwa lengo la kufanya usafi Manispaa ya Iringa ni kuendeza kufanya vizuri kwenye utunzaji na uhifadhi wa mazingira yanayowazunguka jambo ambalo limeutakangaza mkoa wa Iringa kuwa mkoa unafanya vizuri kwenye utunzaji na usafi wa mazingira nchini.
Alisema kuwa wafanyabiashara kufanya usafi ni lazima na inakuaje unafanya biashara kwenye mazingira machafu ambayo utasabasha magonjwa mbalimbali kwa jamii.
Ngwada alisema kuwa Iringa ni mmoja ya mikoa ambayo inaongoza kwa kufanya usafi na ndio jadi ya wanairinga.
No comments:
Post a Comment