MAKAMU RAIS DKT. MPANGO AWAKABIDHI BENKI YA NMB CHETI - UWEZESHAJI WIKI YA UBUNIFU KITAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 21 May 2022

MAKAMU RAIS DKT. MPANGO AWAKABIDHI BENKI YA NMB CHETI - UWEZESHAJI WIKI YA UBUNIFU KITAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango akikabidhi Cheti kwa Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa Benki ya NMB, Josina Njambi na Mkuu wa Idara za Serikali na Ofisi ndogo za Makao Makuu Dodoma wa NMB, Vicky Bishubo kwa kutambua mchango wa benki hiyo kwa kuendeleza shughuli za ubunifu, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa, iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia-Profesa Adolf Mkenda.

Maafisa wa NMB katika picha ya pamoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa, iliyofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameikabidhi Benki ya NMB cheti cha kutambua mchango wa benki hiyo katika kuendeleza shughuli za ubunifu nchini kwa kuwa moja ya wadhamini waliowezesha maonesho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa NMB, Josina Njambi pamoja na Mkuu wa Idara huduma za serikali na Ofisi ndogo za Makao Makuu Dodoma wa NMB, Vicky Bishubo wakati wa kuwapatia vyeti wadhamini mbalimbali pamoja na wabunifu.

Aidha, kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Makamu wa Rais Dkt Mpango alitembelea banda la NMB ambapo alielezwa na Mkuu wa Idara ya Ubunifu, Josina Njambi kuhusu fursa ambayo benki ya NMB imewaletea wabunifu kupitia mfumo wa NMB Sandbox Environment.

“Tumewaletea mfumo huu kwa kuwapa nafasi wabunifu wenye suluhishi za kifedha kufanyia majaribio ya masuluhisho yao na kisha kuwasaidia wabunifu hawa kuingia sokoni.” alisema Josina na kuongeza kuwa;

"Mpaka sasa wapo wabunifu zaidi ya 150 ambao wanaendelea kufanya majaribio ya suluhishi zao mbalimbali," alisema Josina.

No comments:

Post a Comment