FUNGENI NDOA - PADRI MAPALALA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 23 May 2022

FUNGENI NDOA - PADRI MAPALALA

 


Na Adeladius Makwega - DODOMA

WAKRISTO wametakiwa kuacha kuishi maisha ya bila ya kufunga ndoa na wafunge ndoa maana kubadilika kwa tabia ya binadamu huwa si jambo la muda mrefu au mfupi bali ni jambo la maamuzi tu kwa mhusika huyo.

Kauli hiyo imetolewa na Padri Paul Mapalala katika misa ya kwanza ya jumapili ya sita ya mwaka C ya Pasaka katika Kanisa la Bikira Maria Imekulata Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

“Pale unapoamua kuwa sasa mimi ninaachana na jambo baya, ukidhamilia kuacha nalo, unaachana nalo vizuri tu, kwa hiyo unapoamua kubadilika hahitaji muda wowote, tubadilike. Kubadilika kwa tabia ya mtu kutoka kufanya mabaya na kuwa mwema ni dalili nzuri ya mageuzo. Kama wale wenzetu wanaoishi bila ya ndoa kama wanapendana kweli, wafunga ndoa.”

Wapo wanaojaliwa kukaa pamoja miaka sita, saba, nane, tisa hadi kumi na wamebarikiwa kupata neema tele ikiwamo kupata watoto lakini hawafungi ndoa, jamani fungeni ndoa alisisitiza, kiongozi huyo wa kiroho.

“Wanadamu tumekuwa tukipepesa kwa mdomo juu ya upendo lakini ndani ya mitima (roho) yetu kumejaa chuki kubwa. Jamani jambo hilo Mungu hapendi, tupendane kwa matendo yetu na siyo maneno.”

Aliongeza kuwa kwa sasa wazazi wengi hawapo kwenye maisha ya ndoa, jambo hilo linasababisha hata katika jimbo la Kuu Katoliki la Dodoma parokia zake nyingi zimekuwa na watawa mmoja mmoja, kama wazazi wakiwa katika ndoa tutaweza kupata mapadri wengi ambao wanahitajika mno.

Misa hiyo iliambatana na maombi kadhaa ambapo yaliombea wakristo kuishi katika maisha ya ndoa na vijana kujitokeza katika miito ya utawa.

Huku nyimbo kadhaa ziliimbwa kwa uchangamfu na kwaya kutoka Kigango cha Vikonje ambacho ni kigango kimojawapo katika parokia ya Chamwino Ikulu.


No comments:

Post a Comment