RAIS SAMIA HASSAN AMUAPISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE NA BALOZI WA TANZANIA MALAWI, IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 15 March 2022

RAIS SAMIA HASSAN AMUAPISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE NA BALOZI WA TANZANIA MALAWI, IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.



No comments:

Post a Comment