MBUNGE AYSHAROSE ATOA HAMASA KWA WANAFUNZI WILAYA YA IKUNGI, AWAPA TAULO...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 8 March 2022

MBUNGE AYSHAROSE ATOA HAMASA KWA WANAFUNZI WILAYA YA IKUNGI, AWAPA TAULO...!

Mbunge wa Viti Maalum ( CCM)  Mkoa wa Singida Mhe. Aysharose Mattembe (katikati) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Unyahati (hawapo pichani) ikiwa ni moja ya shughuli yake aliyoifanya katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake ambayo kililele chake kitakuwa kesho. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe Miraji Mtatturu, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe na  Diwani wa Viti Maalumu Ikungi, Margaret Chima na baadhi ya viongozi.

 Mbunge wa Viti Maalum ( CCM)  Mkoa wa Singida Mhe. Aysharose Mattembe (katikati) akiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Unyahati baada ya kuwapatia taulo za hedhi ikiwa ni moja ya shughuli yake aliyoifanya katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake ambayo kililele chake kitakuwa kesho. Wengine kutoka kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu Ikungi, Margaret Chima na kulia ni Katibu wa Mbunge Mattembe, Mariam Ntembo.

 Mbunge wa Viti Maalum ( CCM)  Mkoa wa Singida Mhe. Aysharose Mattembe (Wa tatu kutoka kushoto) akiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Unyahati baada ya kuwapatia taulo za hedhi. Kutoka kulia ni Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe na Diwani wa Viti Maalumu wa Ikungi, Margaret Chima.

Furaha ikitawala kwa wanafunzi hao baada ya kupatiwa taulo hizo.

Mbunge Aysharose Mattembe akionesha furaha yake kwa wanafunzi hayo.  

Na Dotto Mwaibale, Singida

KUELEKEA Sikukuu ya Wanawake Duniani ambapo kilele chake ni kesho Machi 8, Mbunge wa Viti Maalum ( CCM)  Mkoa wa Singida Mhe. Aysharose Mattembe  ametembelea  Shule ya Sekondari Unyahati  Wilaya ya Ikungi mkoani Singida. 

Akizungumza katika ziara ya kutembelea shule hiyo ikiwa ni moja ya shughuli yake katika kuadhinisha sikukuu hiyo Mhe Mattembe alisema pamoja na mambo mengine ziara yake hiyo imelenga kuzungumza  na wanafunzi wa kike wa shule hiyo ikiwa ni kuwatia moyo ambapo amewataka wasome kwa bidii. 

"Nawaombeni someni kwa bidii ili mutimize ndoto za maisha yenu kwa kuiga mfano wa Rais wetu Mama Samia Suluhu ambaye alisoma kwa bidii na kuzingatia masomo huku akiwa mtiifu na hatimaye leo hii ni Rais wa kwanza Mwanamke katika katika ukanda wa Afrika Mashariki" alisema Mattembe. 

Mattembe aliwaambia wanafunzi hao kuwa kama watoto wa kike wanawajibu wa kuutambua utu wao, kuthubutu, kujithamini na kujiamini kwamba wanaweza. 

Mbunge Mattembe ametumia nafasi hiyo kugawa taulo za kike kwa wanafunzi hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa hamasa na kutoacha kwenda shule wakati wanapokuwa katika siku zao za hedhi. 

Mattembe alisema kauli mbiu ya sherehe za maadhimisho ya mwaka huu ni Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu" 

No comments:

Post a Comment