ZAWADI ZA NMB MASTABATA KIVYAVYAKO ZAFIKIA MIL. 80 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 25 February 2022

ZAWADI ZA NMB MASTABATA KIVYAVYAKO ZAFIKIA MIL. 80

JUMLA ya Sh Milioni 80,000,000 zimetolewa na Benki ya NMB kwa wateja 80 waliojishindia katika droo ya  MastaBata Kivyakovyako.

Draw ya 8 ya shindano la MastaBata kivyakovyako limechezeshwa jijini Dodoma na Benki ya NMB kwa wateja wanaotumia kadi za Mastercard kwa ajili kufanya miamala popote nchini.

Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB tawi la Kambarage Jijini Dodoma Shukuru Mhagama ambako droo hiyo imefanyika Shukuru Mhagama, alisema walianza Desemba 24,2021 na droo itahitimishwa Machi 23,2022.

Mhagama amesisitiza Wateja wanaotumia NMB Mastercard kufanya malipo kwenye POS, QR au mitandaoni ndiyo ambao wanaingia kwenye droo hiyo.

Kila wiki wanapata washindi 100 ambao kila mmoja anajishindia kitita cha Sh100,000, kuna washindi 25 wa mwezi ambapo kila mmoja anashinda Sh Milioni 1 na mwisho wa shindano kutakuwa na droo kubwa ya washindi 30 kuondoka na Sh Milioni 3.

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Ibrahim Sikana alisema hakujawahi kuwa na kelele wala malalamiko katika droo zote za NMB hivyo wanaamini kila jambo huendeshwa kwa utaratibu ndani ya benki hiyo.

Meneja wa Tawi la Kambarage, Emiliana Wilson aliwataka wateja kuendelea kuiamini Benki ya NMB na kuitumia kwani ni Benki pendwa inayotoa huduma zake katika maeneo mengi nchini.

No comments:

Post a Comment