TMA, NEMC WASHIRIKIANA KUTOA ELIMU JUU YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WADAU WA MAZINGIRA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 18 February 2022

TMA, NEMC WASHIRIKIANA KUTOA ELIMU JUU YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WADAU WA MAZINGIRA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jafo, akizungumza na wadau wa mazingira alipokuwa akifungua warsha ya kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira. Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya NEMC, TMA pamoja na Chama cha Wataalam wa Mazingira (TEEA) imefanyika leo Ukumbu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kulia) ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) akizungumza kwenye warsha ya kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira. 

Mkurugenzi wa Tathimini ya Athari kwa Mazingira (NEMC), Lilian Lukambuzi, akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jafo (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kulia) ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwenye warsha ya kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira. 

Mwakilishi kutoka Chama cha  Wataalam wa Mazingira, (TEEA), akizungumza katika mkutano huo.

Wataalam wa hali ya hewa kutoka TMA (mbele) pamoja na washiriki katika warsha ya kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira wakifuatilia masuala mbalimbali.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jafo, akisisitiza jambo kwa wadau wa mazingira alipokuwa akifungua warsha ya kujenga uelewa kuhusu taarifa za Hali ya Hewa, fursa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau wa mazingira. Warsha hiyo imefanyika leo Ukumbu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment