Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith .Mahenge akitoa maelezekezo wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama aliyoifanya jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos. Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mtaa Mkoa wa Singida Evodius Katale na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ametoa siku 15 kuhakikisha Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika Halmashauri za Wilaya za Mkalama,Ikungi pamoja na jengo la Halmashauri ya Wilaya la Singida DC kukamilisha haraka ujenzi huo ili watumishi waweze kuanza kuishi kwenye nyumba hizo na kuipunguzia Serikali gharama.
Dk.Mahenge aliyasema hayo jana kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya siku moja kwenye wilaya hizo ya Kukagua ujenzi wa majengo hayo ambapo hakuridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa miradi na akawaagiza wakandasi kuongeza kasi.
"Natoa muda wa siku 15 hadi ifikapo Februari 15, 2022 watumishi wote wawe wamehamia katika nyumba hizo vinginevyo hawatapata fedha kwa ajili ya pango" alisema Mahenge.
Miradi iliyokaguliwa na Dk. Mahenge ni ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama unaotekelezwa na Wakala wa Majengo (TBA) ambao thamani yake ni Sh.1,,331,907,458.00 ambao ujenzi wake umekuwa ukisuasua kutoka na mkandarasi huyo kutopata fedha kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali.
Mradi mwingine ni ni ujenzi wa ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambao Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 iliidhinisha kiasi cha Sh.1,000,000,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa awamu ya kwanza ambao unatekezwa kwa mfumo wa Force Account.
Mradi wa tatu uliokaguliwa na Dk.Mahenge ni ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi unaotekelezwa na Kampuni Tanzu ya Mzinga (Mzinga HoldingCompany Limited ya Morogoro) wenye thamani ya Sh.1,392,649,148.94 ambapo mkandarasi huyo tayari amelipwa Sh.698,814,485.18.
No comments:
Post a Comment