CCM SINGIDA YAIPONGEZA WILAYA YA SINGIDA DC KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 29 January 2022

CCM SINGIDA YAIPONGEZA WILAYA YA SINGIDA DC KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo  Kata ya Msange Wilaya ya Singida DC jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC Ester Chaula.

Mwenyekiti wa CCM  Kata ya Msange Joel Ndweti akizungumza kwenye ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC. William Nyalandu.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo akizungumza kwenye ziara hiyo Kata ya Msange.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Ester Chaula akichangia jambo wakati akielezea ukarabati wa madara katika Shule ya Msingi Msange.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati wa ziara hiyo Kijiji cha Mangida.

Mzee maarufu wa Kata ya Msange Philemoni Mnyawi (kushoto) kwa niaba ya wazee wa kata hiyo akimvika shuka Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC. William Nyalandu kama ishara ya heshima ya kimila kwa kabila la Wanyaturu wakati wa ziara.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhajj Killimbah akivikwa shuka la heshima.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Idara ya Oganaizesheni Dafroza Lucas akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jangwa katika ziara hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa  wilaya hiyo wakiwa nyumbani kwa Mzee maarufu wa Ilongero na muasisi wa CCM, Seif Muhomi ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana  kwa ajili ya kutoa rambirambi.



wajumbe wa kamati hiyo ya utekelezaji ya wilaya hiyo wakiwa Shule ya Msingi ya Msange wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC William Nyalandu akizungumza kwenye ziara hiyo.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Msange Mariam Wela akisoma taarifa ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo.

Muonekano wa madarasa ya Shule ya Msingi Msange baada ya kukarabatiwa.

Zawadi ya mbuzi ikitolewa kwa Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida.

Zawadi zikitolewa.

Zawadi zikitolewa.

Zawadi zikitolewa.

Ukaguzi wa madarasa Shule ya Msingi Msange ukuendelea.
Ukaguzi wa vyoo Shule ya Msingi, Jangwa ukiendelea.
Wananchi wa Kijiji cha Jangwa wakiwa kwenye mkutano wakati wa ziara hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Jangwa wakiwa kwenye mkutano wakati wa ziara hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi  Jangwa Jumanne Mangu akisoma taarifa ya shule hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mzee Philemoni Mnyawi akionesha furaha yake kabla ya kutoa zawadi kwa baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ziara hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Madasenga akitoa taarifa ya ujenzi  wa madarasa katika shule hiyo. 
Ukaguzi wa shule hiyoukiendelea.
Wakina mama wa Kijiji cha Mangida wakitoa burudani wakati wa ziara hiyo. 
Mkutano katika ziara hiyo Kijiji cha Mangida ukiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mangida wakiwa kwenye mkutano wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mangida wakati wa ziara hiyo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa wilayani humo.

Kilimba ametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana ya kukagua miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) na kufanya mikutano na wananchi ilikujua changamoto walizonazo na kuzitafutia utatuzi.

Kilimba alitoa pongezi hizo baada ya kuridhishwa na utekelezwaji wa ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Msange ambayo yalikuwa katika hali mbaya na kushindwa kutumika kutokana na uchakavu.

"Nilifika hapa miezi mitatu iliyopita nikiwa na wajumbe wa kamati ya siasa mkoa ambapo madarasa haya tuliyakuta yakiwa katika hali mbaya ndipo nilipotoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatafuta fedha kwa ajili ya kuyakarabati na mshukuru sana mkurugenzi huyo kwa kutekeleza agizo hilo baada ya kutoa fedha Sh. 17,500,000 kutoka mapato ya ndani na kukamilisha ujenzi huo" alisema Killimbah.

Akizungumza wakati akiendelea kukagua miradi aliipongeza wilaya hiyo kwa kuitendea haki miradi  ambayo Serikali imetumia fedha nyingi kuitekeleza hasa ujenzi wa madarasa yaliotokana kwa fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19.

Kilimba alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwan kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Killimbah alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ambayo kwa mkoa mzima zimetumika Sh.13.4 kumewaondolea adha ya kusoma katika mazingira yasiyo rafiki kwa wanafunzi kuanzia shule shikizi, msingi na sekondari.

Alisema hivi sasa nchini kote baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kubwa ya kutoa fedha hizo wananchi hawazungumzii tena ujenzi wa madarasa au ukosefu wa madawati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Aidha Killimbah alisema mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa ndani wa viongozi watakaoshika nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya mashina, vitongoji, kata, wilaya  hadi mkoa ambapo aliwaomba Wana CCM wote kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo alimpongeza Kilimbah kwa ufuatiliaji wa ahadi yake kama alivyoahidi kurudi kuyagua tena madarasa ya shule hiyo ya Msange na kuwa kazi hizo za maendeleo zinazofanyika ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwa wataendelea kufanya hivyo.

"Tutaendelea kuwatumikia wananchi kwa kufanya kazi za maendeleo na nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali" alisema Ighondo. 

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Idara ya Oganaizesheni Dafroza Lucas akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jangwa katika ziara hiyo aliwahimiza wakati wa zoezi la Sensa ya watu na makazi litakapo wadia mapema mwaka huu wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.

Baadhi ya  miradi iliyokaguliwa na Mwenyekiti huyo wa CCM ambaye aliambatana na kamati ya utekelezaji ya wilaya hiyo ni mradi wa ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Msange, kukagua kukamilika kwa madarasa ya Uviko Shule ya Sekondari ya Madasenga iliyopo Kijiji cha Mangida na Shule ya Msingi ya Jangwa ambayo inachangamoto kubwa ya kutokuwa na vyoo.

Killimbah katika ziara hiyo alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Mangida, Sefunga na Hendeshi ili kujua changamoto zao ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

Katika hatua nyingine kabla ya kuanza kwa ziara hiyo Killimbah pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ya utekelezaji ya wilaya hiyo walikwenda kutoa rambirambi nyumbani kwa Mzee maarufu wa Ilongero na muasisi wa CCM, Seif Muhomi ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana.

No comments:

Post a Comment