Na Dalphina Rubyema, Kigoma
VIONGOZI wa Dini mkoani Kigoma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo mkoani humo wamekutana na kujadili kwa pamoja, mustakhabali wa mwitikio wa jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) na suala la Usawa wa kijinsi ikiwa ni utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Majadiliano hayo yameratibiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kupitia Mradi wake wa Uimarishaji wa Asasi za Kiraia kwa kushirikiana na Kamati ya Mahusiano ya Dini Mbalimbali mkoani Kigoma chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada kwa Makanisa la Norway (NCA).
Akifungua Mjadiliano hayo, Mwenyeketi wa Kamati ya Mahusiano ya Dini Mbalimbali mkoani Kigoma, Sheikh Hassan Idd Kiburwa, amewataka viongozi wa dini kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha na kuiongoza jamii ili ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe imeboresha afya za Watanzania na kujenga usawa wa kijinsia.
“Penye umasikini tambua kwamba nyuma yake kuna kiongozi mbovu…na matokeo ya umasikini ni huduma mbovu za afya na unyanyasaji wa kijinsia kwani familia na jamii kwa ujumla, hivyo sisi kama viongozi wa dini ni wajibu wetu kuhakikisha mambo haya yanaondolewa hadi kufikia 2030,” amesema.
Kiini cha majadiliano haya kwa mujibu wa Afisa Mradi huo, Bi. Joyce Lusatila ni upimaji wa utekelezaji wa maazimio ya semina ya mafunzo juu ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Haki za Binadamu hususan malengo namba namba 1, 2,3,5,10 na 16 iliyotolewa kwa nyakati mbalimbali kwa wadau wa maendeleo katika Wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu, Buhigwe, Uvinza na Kigoma Mjini.
Amesema baada ya mafunzo hayo yaliyoratibiwa na TEC kwa kushirikiana na Kamati ya Dini Mbalimbali katika wilaya husika, kila wilaya ilichaugua lengo mojawapo kwa ajili ya kulifanyika utafiti ambapo Wililaya za Kakonko, Kasulu na Kibondo zilichagua lengo namba tatu inayohusu Afya na Ustawi na zaidi ziliangalia suala la Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) huku Wilaya za Kigoma na Uvinza kichagua lengo namba tano inayohusu Usawa wa Kijinsia.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye kituo cha Nzimano Jimbo Katoliki Kigoma na kuwashirikisha wadau wa maendeleo wakiwemo viongozi wa dini, mashirika ya kiraia yanayofanya kazi mkoani humo na viongozi wa watendaji wa serikali, unatoa fursa kwa kamati za Mahusiano ya Dini Mbalimbali katika wilaya husika, kuwasilisha kile walichobaini hatimaye vyombo vya kimamlaka kutoa ufafanuzi na kufikia hitimisho la pamoja.
Wakati Mwenyekeiti wa Kamati ya Mahusiano ya Dini Mbalimbali wilayani Kakonko, Padri Joseph Huriro akisema kamati yake ilikichagua Kijiji cha Kasongati kama eneo lake la kujifunza mwitiko wa iCHF kwa jamii, Mwenyekiti wa Kamati wilayani humo Mch, Brighton Kibabi, anasema kamati ilichagua Kijiji cha Heruju huku Padri Madugu Gulasiano Mwenyekiti wa Kamati ya Wilaya ya Kibondo anasema wao walichagua Kijiji cha Nyange.
Upande wa Kakonko hadi kufikia Julai 10 mwaka huu idadi ya wanachama waliokuwa wamejiunga na iCHF katika Kijiji cha Kasongati ni 196 katik ya wakazi wote wapatao 4,381( sawa na asilimia 4.5), lakini baada ya uhamasishaji mwitikio uliongezeka na kufikia asilimia 9 na hii ni kwa mujibu wa Oktoba 10 mwaka huu.
Katika Kijiji cha Herujuu wilayani Kasulu, kabla ya uhamasishaji idadi ya wanachama wa iCHF ilikuwa ni 4.1 lakini baada ya uhamasishaji wanachi wameonesha mwitikio chanya hivyo idadi kuongezeka na kufikia 7.9 huku Kijiji cha Nyange hadi kufikia Oktoba 10 mwaka huu idadi ya wanancha wa mfuko huo ilikuwa ni 5.6
Viongozi hao wanataja baadhi ya sababu zinazochangia wananchi kusuasua kujiunga na iCHF kuwa ni pamoja na uelewa mdogo, kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na mfuko huo likiwemo suala la ukosefu wa dawa, lugha isiyofaa, uaminifu mdogo katika zoezi la uandikishaji ambapo baadhi ya waandikishaji wamekuwa wakichukua hela ya wananchi pasipo kuwaandika kwenye kitabu cha usajili pamoja na mlolongo katika kutoa rufaa kwa wagonjwa.
Upande wa Usawa wa Kijinsia, wawakilishi wa Wilaya ya Uvinza na Kigoma kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano Wilayani Uvinza, Sheikh Hassan Isa Mkuya , amebainisha kwamba, bado kuna unyanyasaji wa kinjinsia iwe ni wa kingono, kiuchumi, kisaiklojia na kwamba katika kipindi cha mwaka 2015/2016 takribani wanawake 1,652 mkoani Kigoma walikuwa wamefanyiwa ukatili na chanzo cha ukatili huu ni umasikini, matumizi mabaya ya madara, wivu wa kimapenzi.
Katika kuchangia hoja hii Afisa Ustawi wa Jamii na Mratibu wa iCHF Mkoa wa Kigoma, Bw. Elisha Nyamala, anasema kutokana na hali ngumu za kiuchumi, uenda baadhi ya wananchi wanashindwa kupata hela ya kujiunga na mfuko huo, hivyo akapendekeza shughuli ya uhamasishaji ikaangali msimu ana kipindi gani cha mwaka kufanya uhamasishaji huo.
Kuhusu suala la lugha chafu na huduma mbuvu kwa wanachama wa iCHF, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Oseh William, anasema hilo ni suala la kinidhamu na kusema kwamba ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) ina kitengo cha malalamiko, hivyo akawataka wakaotendewa kinyume wawasilishe mamamiko yao ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Katika kuchangia hoja za usawa wa kijinsia,Mratibu wa Dawati la Jinsia mkoani Kigoma, Annastazia Daudi, anaanza kwa kuwataka viongozi wa dini kujitathmini hususan suala la umri wa mtoto kuolewa au kuoa, kwa kile anachosema unakindhana na sheria ya nchi.
Katika mapendekezo yao, washiriki hao wamesema viongozi wa dini wanatakiwa kuendelea kuelimisha jamii juu ya iCHF huku upande wa utawala ukitakiwa kufanya ufuatiliaji/ ukaguzi wa daftari la wanachama wa iCHF na kumchukulia hatua mwandikishaji atakayebainika kudhurumu hela za wanachama, kuongeza idadi ya watumishi wa iCHF.
Mapendekezo mengine ni kutafuta namna ya kukata hela iCHF wakati wa msimu wa mavuno, kufanya ufuatilia na kutoa adhabu kwa maduka ya dawa yanayofifisha bima ya afya pamoja na kamati za maadili katika vituo vya afya kupewa meno na zaidi.
No comments:
Post a Comment