Askofu Ndabila akiwa kwenye maombi hayo.
Mke wa Askofu Ndabila Janeth Ndabila akifanya maombi ya kuliombea Taifa.
Maombi yakiendelea.
Maombi yakifanyika.
Askofu Ndabila (kushoto) akiwa kwenye maombi hayo.
Waumini na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wakiwa katika maombi.
Maombi yakifanyika.
Wanakwaya wa Kanisa hilo wakiwa kwenye maombi.
Maombi ya kuliombea Bara la Afika yakifanyika.
Picha ya pamoja baada ya kufanyika maombi hayo.
Na Dotto Mwaibale
KANISA la Abundant Blessing Center (ABC) la Tabata jijini Dar es Salaam limefanya maombi maalumu ya kuliombea Taifa na kumshukuru Mungu kwa kumpa ulinzi Rais Samia Suluhu Hassan.
Maombi hayo yaliongozwa na Askofu Kiongozi wa Kanisa hilo Flaston Ndabila kwa kushirikiana na wakristo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika maombi hayo Askofu Ndabila aliwasisitiza viongozi wa kikristo na wakiristo wote kushiriki maombi ya kushukuru na kuitamkia nchi yetu mema kila jumamosi ya tatu ya mwezi kwa kushirikiana na wakristo wote dunia ambapo pia aliishukuru huduma ya IGO Africa For Jesus Prayer Movement kwa kuwaunganisha wakriso ulimwenguni kote kufanya maombi hayo.
"Nimpongeza Dkt. Nicku Kyungu Mordi mtanzania aishie Marekani kwa kuiongoza huduma hii ya Igo Africa For Jesus Prayer Movement kwa miaka 28" alisema Ndabila.
Aidha Ndabila alimshukuru Mungu kwa kuliwezesha taifa letu kuwa na amani na utulivu na kutekeleza miradi yote ya maendeleo.
Ndabila alimuomba Mungu aliepushe taifa letu na Afrika kwa ujumla na vitendo vya ugaidi na kuilinda mipaka yetu ili amani iendelee kutamalaki nchini.
Pia Ndabila alimuomba Mungu atuepushe na vitendo vya ushoga, usagaji, ulawiti, utumiaji wa dawa za kulevya, ulevi, rushwa na maovu mengine.
Ndabila alivitaka vyombo vinavyosimamia sheria, polisi, mahakama, usalama wa taifa kutenda haki na akamuomba Mungu awape hekima waliopewa dhamana hiyo wafanye kazi zao kwa hofu ya Mungu.
Mchungaji wa Kanisa la ABC Kibaha, Lois Malali akiongoza maombi ya kumshukuru Mungu kumpa ulinzi Rais Samia alisema kama kanisa wanaamini Mungu ataendelea kumlinda dhidi ya maadui wa nchi yetu.
“Tumuombee Rais wetu Samia Suluhu Hassan moyo wa hekima, busara na ustahimilivu wa kuweza kupambanua mema na mabaya kwa ajili ya nchi yetu,” alisema Malali.
Mchungaji Msaidizi wa Uamusho wa Kanisa la Pentekosti la Shekilango jijini Dar es Salaam, Mupana Venuster alimshukuru Mungu kwa ajili ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baraza la mawaziri, majaji, mahakimu, Spika wa Bunge Job Ndugai na wabunge kwa kuiongoza vyema nchi yetu.
Venuster alimuomba Mungu awajalie hekima ya kulipenda taifa letu na kuwa na nia ya kulijenga.
“Mungu awape ulinzi maalumu kwa wanaofanya mambo ya kuwasaidia wananchi iwe kwenye idara za serikali, mahakama, bunge awajalie kukataa mikataba na maamuzi mabaya ya kuliangamiza taifa letu,” alisema Venuster.
Mchungaji Jema Fungo wa Huduma ya Maombi Kibaha alimshukuru Mungu kwa kutupatia mvua za masika na vuli tangu nchi yetu ilipopata uhuru miaka 60 iliyopita na kumsihi afanye hivyo katika kipindi hiki na azibariki kazi za mikono yetu.
Fungo alimuomba Mungu atupe mvua ya neema isiyokuwa na madhara na amani itawale kwenye mipaka yetu na nchi yetu isikumbwe na njaa.
Mke wa Askofu Ndabila, Janeth Ndabila akiongoza maombi ya kuiombea jamii alimsihi Mungu awaondoe watu wabaya wanaotaka kuiharibu jamii ya kitanzania hususan vijana wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.
“Tunaikataa hali inayoendelea sasa katika mitandao ya kijamii na familia, maneno yasiyofaa ya kujipendekeza bila kujali madhara yake na maneno ya unafiki,” alisema Ndabila.
Lyidia Mcharo wa Huduma ya Maombi alimuomba Mungu awainue vijana ili waamini katika kumtumikia.
Wengine walioshiriki kwenye maombi hayo ni Mchungaji Imani Shukurani, Askofu Price Twail, Mchungaji Joel Juma na Dickson Malali wote kutoka katika Kanisa la ABC.
No comments:
Post a Comment