STAMICO NA NMB WASHIRIKIANA KUWAINUA WACHIMBAJI MADINI NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 22 November 2021

STAMICO NA NMB WASHIRIKIANA KUWAINUA WACHIMBAJI MADINI NCHINI

Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto (kushoto) akibadilishana nyaraka na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse jijini Dar es Salaam, mara baada ya kusaini ushirikiano kibiashara, katika makubaliano hayo NMB itatoa mikopo rafiki kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini kwa ajili ya kuwawezesha kununua vifaa vya uchimbaji. 

Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto (kushoto) akitiliana saini ya ushirikiano kibiashara na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse jijini Dar es Salaam, katika makubaliano hayo NMB itatoa mikopo rafiki kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini wenye sifa kwa ajili ya kuwawezesha kibiashara. Kulia ni Mwanasheria wa STAMICO, Bw. Vicent Lugendo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse (kulia) akizungumza katika hafla ya kutiliana saini ya ushirikiano na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto. Katika makubaliano hayo NMB itatoa mikopo kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini kwa ajili ya kuwawezesha kibiashara. 

Hafla ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) iliyofanyika katika ofisi za STAMICO jijini Dar es Salaam ikiendelea. 

Maofisa waandamizi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakifuatilia mazungumzo hayo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse (kulia) akifafanua jambo kwa wanahabari katika hafla ya kutiliana saini ya ushirikiano na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto.

Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto (wa pili kushoto), pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse (wa pili kulia) wakionesha nyaraka za mikataba waliosaini katika makubaliano ya ushirikiano kati ya STAMICO na Benki ya NMB. 

Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto (kushoto) akitiliana saini ya ushirikiano kibiashara na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse jijini Dar es Salaam, katika makubaliano hayo NMB itatoa mikopo rafiki kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini wenye sifa kwa ajili ya kuwawezesha kibiashara. 


SHIRIKA la Madini Tanzania (STAMICO) limeingia makubaliano kiushirikiano na Benki ya NMB ili iwasaidiwe wachimbaji na wadau wa sekta ya madini kutoa mikopo rafiki ya ununuzi wa vifaa vya uchimbaji na elimu ya fedha kwa lengo la kuwainua katika shughuli zao.

Wakizungumza katika hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano huo, Afisa Mikopo Mkuu wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Bw. Daniel Mboto amesema NMB itashirikiana na STAMICO kuhakikisha inatambua wahitaji wenye sifa na kuwakopesha mikopo rafiki kwa ajili ya kununulia vifaa vya uchimbaji.

Alisema NMB kwa kushirikiana na wataalamu wa STAMICO watawatambua wachimbaji wadogo wenye uhitaji na kuwapa mikopo hiyo ili iweze kuwainua katika shughuli zao za uchimbaji, huku mikopo ikilenga zaidi uboreshaji vifaa na mitambo ya uchimbaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse akifafanua zaidi alisema lengo la shirika ni kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika kikamilifu kwenye shughuli hizo na ndio maana inaendelea kushirikisha wadau taasisi za fedha ili ziweze wakopesha na kuboresha shughuli za uchimbaji kwao.

Aliongeza kuwa STAMICO itaendelea kushirikiana na wadau wengine, katika hatua mbalimbali ili kutoa ushindani wa kibiashara huku ikijikita kuwainua wachimbaji hasa katika uchimbaji wenye tija na uhakika wa wahusika kunufaika na rasilimali hizo. 

"Tumejipanga kununua mashine za kuchoronga miamba kila mwaka ili kuhakikisha tunawasaidia wachimbaji wadogo kutambua maeneo yenye tija na uhakika wa kumnufaisha mchimbaji , tofauti na hapo awali walipokuwa wakipotenga nguvu nyingi hata katika maeneo yasio na uhakika wa rasilimali hiyo," alisema Dk. Mwasse.

No comments:

Post a Comment