ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI MHE. NDAYISHIMIYE NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 22 October 2021

ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI MHE. NDAYISHIMIYE NCHINI


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021. PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye aliyekuwa akiongoza ujumbe kutoka Burundi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali mara kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakati nyimbo za Mataifa mawili Tanzania na Burundi pamoja na wimbo wa Afrika Mashariki  zikipigwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye  mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba, 2021 kwa ziara ya kikazi ya siku 3.

No comments:

Post a Comment