TANZANIA YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MATAIFA DUNIANI KATIKA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 21 October 2021

TANZANIA YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MATAIFA DUNIANI KATIKA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Gerlad Kusaya akiwa na ujumbe wake wakishiriki katika mkutano wa 64 wa majadiliano ya majadiliano ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani ulioanza Oktoba 18 - 21 Mwaka huu Jijini Vienna Nchini Austria.

Na Mwandishi Wetu, Vienna Nchini Austria

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya akiambatana na maafisa wengine ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa 64 wa Majadiliano ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani ulioanza Oktoba 18 - 21 Mwaka huu Jijini Vienna Nchini Austria.


Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.


Pia, Mkutano huo ulijadili namna bora ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya na makosa mengine ya uhalifu wa kupangwa ikiwepo ya Ugaidi, Utakatishaji fedha, Usafirishaji haramu wa Binadamu na Uhalifu wa kimtandao na kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja nakutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Duniani.


No comments:

Post a Comment