WAKULIMA WANUFAIKA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MOMBO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 20 September 2021

WAKULIMA WANUFAIKA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MOMBO


Picha ikionesha sehemu ya shamba la mpunga katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mombo.

Picha ikionesha Mfereji wa upili unaopeleka maji mashambani katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Mombo.

Na Mwandishi Wetu, Mombo 

WAKULIMA katika siku ya kilimo cha Umwagiliaji Mombo Wilayani Korogwe, wamenufaika na Kilimo hicho baada ya Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuwajengea miundombinu inayopeleka maji mashambani pamoja na kuwajengea maghala ya kuifadhia mazao,kupata elimu ya kuongeza thamani ya zao la mpunga linalolimwa katika katika skimu hiyo pamoja na elimu ya mafunzo na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika skimu hiyo baadhi ya wakulima wamesema kuwa, kupitia kuwepo kwa miundombinu thabiti katika mashamba hayo, wameweza kulima kilimo cha teknolojia mpya, na kuongezeka kwa pato la mkulima mmoja mmoja, kujenga na kuishi katika nyumba za kisasa pamoja na kumudu kuwapeleka watoto shule.

Bwana Hamis Said mwenyekiti wa ushirika wa wakulima katika skimu hiyo alisema sambamba na faida wanayoipata kutokana na kilimo katika skimu hiyo wameweza kupata elimu kuhusu uchangiaji wa ada za huduma ya umwagiliaji pamoja na utekelezaji wake.

Skimu ya Kilimo cha umwagiliaji Mombo ina ukubwa wa eneo la hekta 220, zinazotumika katika kilimo cha umwagiliaji katika misimu miwili kwa mwaka yaani kiangazi na vuli ambapo jumla ya wakulima 429 wanajishughulisha katika shuguli za kilimo cha umwagiliaji.

No comments:

Post a Comment