KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kubangua Korosho kinachojengwa kwenye Kijiji cha Nkanyevi Kata ya Sigaya wilayani Mkinga ambapo hatua hiyo inatokana na jitihada za kampuni mama ya Out-Growers Tanzania Limited ambayo muasisi wake ni Karstern Solaas Raia wa Denmark.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Out Growers Tanzania Limited Reginali Mpolo akielezea jambo wakati wa ziara hiyo.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred katikati akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Mkinga mkoani Tanga ambapo alitembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kubangua Korosho kinachojengwa kwenye Kijiji cha Nkanyevi Kata ya Sigaya wilayani Mkinga kulia ni Meneja wa Bodi ya Korosho Mkoa wa Tanga Ugumba Kilasa.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kiwanda hicho kushoto ni Meneja wa Bodi ya Korosho Mkoa wa Tanga Ugumba Kilasa.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred kushsoto akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Out Growers Tanzania Limited Reginali Mpolo wakati wa ziara hiyo (aliyevaa rifleta) mara baada ya kuwasili katika eneo la ujenzi huo.
umwagakji kokote ukiendelea.
NA OSCAR ASSENGA, MKINGA
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema wataanzisha kampeni ya ufufuaji wa mashamba ya Korosho mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na mamlaka za mkoa na wilaya kwa kuandaa mpango mahususi ambao watapita wilaya moja hadi nyengine ambazo zinalima zao hilo.
Aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Tanga ambapo alitembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kubangua Korosho kinachojengwa kwenye Kijiji cha Nkanyevi Kata ya Sigaya wilayani Mkinga ambapo hatua hiyo inatokana na jitihada za kampuni mama ya Out-Growers Tanzania Limited ambayo muasisi wake ni Karstern Solaas Raia wa Denmark.
Kiwanda hicho kinajengwa kwa mkoa kutoka Benki ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na hisa za Ubia za Kampuni ya Out-Growers Tanzania Limited chini ya usimamizi wa ujenzi kutoka kampuni ya NOLC Engineering Co.Limited na unakadiriwa kuwa na thamani ya Milioni 450,000,000 na utakamilika mwezi Desemba mwaka 2021.
Alisema lengo la wao kupitia huko ni kuwahimiza na kuhamaisisha wakulima waweze kufufua zao lao kwa sababu wana uhakika wa soko zao hilo kutokana na kwamba Tayari wana kiwanda eneo la Mkinga ambacho kitakuwa na uwezo wa kununua zao hilo na zile changamoto zao za soko zitakuwa zimepungua.
Alisema wakulima hao wataweza kuuzia korosho zao mahali penye uhakika na hisa ambazo wakulima kwenye kiwanda hicho hawatazilipa mara moja kutokana na faida ambazo wanazipata mwishoni kwa hiyo wataendela kulipa kama kawaida na wataweza kununua hisa zao kidogo kidogo kupitia faida zinazopatikana kupitia kiwanda hicho.
“Kwa kuanzia kiwanda hiki kitakuwa kinauwezo wa kubangua Korosho tani 300 lakini wamesema wanawezaa kuongeza hadi tani 600 maana yake wataweza kubangua asilimia 50 ya korosho zote za mkoa wa Tanga kitu ambcaho ni hatua kubwa sana,” Alisema.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema ili kuhakikisha ubangua huo unafanikiwa kwa mkoa wa Tanga huo watakuwa wakihamasisha vikundi vidogo vidogo vya ubanguaji kubangua hatua ya awali ili kukiwezesha kiwanda hicho kiweze kuchukua korosho hizo na kutafuta masoko.
“Lakini niwaambie kwamba Mwekezaji wa kiwanda hiki anatokea Denmark na tuna uhakika ubanguaji wa korosho kwenye kiwanda hiki utafungua milango ya soko la korosho kwenye nchi hivyo hilo ni jambo muhimu kwa sababu litafungua soko la ulaya,” Alisema.
“Tutahamasisha wakulima wa mkoa wa Tanga kufufua mashamba yao na wayahudumie najua mwaka huu hawakupata pembejeo lakini msimu ujao kupitia mpango wa serikali wa pembejeo ambao wakulima watapewa pembejeo kwa njia ya ruzuku na kulipia asilimia 50 Tanga pia itawekwa kwenye mpanmgo huo”Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.
“Nimefurahi kufika Kijiji cha Nkanyevi Kata ya Sigaya wilaya ya Mkinga kwenye kiwanda cha Kubangua Korosho upande wa Mkoa wa Tanga kumekuwa na changamoto ya soko kwa sababu korosho za mkoa wa Tanga zinakoma kipindi ambacho tayari wanunuzi wengi wamekwisha kuondoka mwezi wa pili na wa tatu hivyo wamekuwa wakipata shida namna ya kuuza korosho hivyo ujenzi wa kiwanda hicho kupitia kampni ya Out Growes ni hatua moja kubwa sana,” Alisema.
Hata hivyo aliipongeza kampuni hiyo kwa kufikia hatua hiyo lakini kiwanda hicho kinajengwa kwa ubia kati ya Out Growes na wakulima wa Korosho wana asilimia 45 kwenye kiwanda hicho kwa hiyo ina maana wakulima wa kijiji cha Duga Amcos na maeneo ya jirani watakuwa wanabangua Korosho kwenye kiwanda chao na hivyo italeta hamasa kwenye zao la korosho kuongeza uzalishaji katika mkoa wa Tanga na kuweza kuboresha korosho zao kuwa bora zaidi.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Out Growers Tanzania Limited Reginali Mpolo alisema ujenzi huo umeanza mwezi wa saba utakamilia Desemba kiwanda na mashine ambazo zinauwezo wa kubangua tani 300 kwa mwaka lakini wanaweza kuongeza mashine zaidi na kubangua hadi tani 600 kwa mwaka.
Alisema wamemua kuazisha kiwanda hicho kwa sababu kuna Raia wa Denmark Karstern Solaas alifika hapo mwanzoni mwa mwaka 2015 kwa lengo la kuwasaidia wakulima wa Tanzania hususani wa Mkinga wa kupata soko la uhakika la Korosho zao na kuweza kushiriki kwenye ujenzi wa kiwanda hicho kuwa na hisa kwa maana ya kwamba malighafi nyingi zinaenda nje ya nchi na kuwaacha watu kutokuwa na ajira.
Alisema wazo hilo lilipelekea akawaita mpaka sasa wameungana na wakulima kupitia Duga Amcos wana asilimia 45 na yeye ana asilimia 51 na mwekezaji mwengine ana asilimia 4 na ujenzi huo ukikamilika utakuwa ni mkombozi kwa wakulima wilaya ya Mkinga na Mkoa wa Tanga.
No comments:
Post a Comment