Na Dotto Mwaibale
WANAMUZIKI Nchini wameanza maandalizi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani yatakayoadhimishwa kitaifa jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel alisema tayari wameanza kuandaa maandalizi kwa ajili ya maadhimisho hayo.
"Tumeanza maandalizi ya Siku hiyo na tayari baadhi ya wanamuziki wamekwisha thibitisha kushiriki,". alisema Joel.
Alisema kuwa leo saa 4 asubuhi katika Hoteli ya Kibo Palace Jijini Arusha watakutana na waandishi wa habari na kuzungumzia kwa kina maandalizi hayo.
Joel aliwataja baadhi ya wanamuziki waliothibitisha kushiriki maadhimisho hayo kuwa ni Komandoo Hamza Kalala, Stara Thomas na wengine wengi.
Alisema kilele cha maadhimisho hayo itakuwa ni Oktoba 1,2021.
No comments:
Post a Comment