SERIKALI YATOA VITI 600 MCSD - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 28 October 2024

SERIKALI YATOA VITI 600 MCSD



Na Adeladius Makwega & Joseph Mbugi-WUSM

SERIKALI imetoa viti vya kukalia mia sita (600) kwa Chuo cha Maendeelo ya Michezo Malya MCSD ambavyo vitatumika kwa matumizi mbalimbali kwa taasisi hii ya umma nchini ambapo ni chuo pekee kinachotoa elimu ya michezo kwa ngazi za astashahada na stashahada kadhaa za michezo.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwa taasisi hii Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Methusela Ntonda amenadi haya huku akisema kuwa serikali inawekeza kwa kiasi kikubwa cha fedha kwa miundo mbinu ya chuo hiki shabaha ni kwa watoto wa Watanzania wasome na kupata fursa za michezo nchini na ulimwenguni.

“Kwa sasa chuo hiki kimepokea fedha kadhaa za miradi ya maendeleo karibu bilioni 40 ni kwa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya sekta ya michezo na miradi yote ipo chini ya udhamini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugezni Msaidizi anayeshugulikia Miundo Mbinu katika wizara hii mkufunzi Alex Mkenyenge amesema viti mia sita kwa MCSD vipo tayari sasa anafanya utaratibu viti hivyo kufika Malya Kwimba Mkoani Mwanza.

Sambamba na hilo, wakizungumza ndani ya kikao hicho huku mawingu, radi , ngurumo na mvua kubwa zikisindikiza shughuli kikao hicho mwanachuo wa kozi ya Elimu ya Vitendo Ramla Teodori aliomba wanachuo wa chuo hiki kupatiwa vifaa vya muziki ili waweze kuvitumia katika mazoezi ya vitendo naye Elifasi Masawe mwanachuo anayesoma Stashahada ya Uongozi katika Michezo aliomba kupatikana kwa maji ya uhakika.

Akijibu maswali haya Naibu Katibu Mkuu Ntonda alisema kuwa haya yote yatafanyiwa kazi mapema.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha MCSD Jaochim Maganga ameshukuru kwa kupatikana kwa viti hivyo na vifaa vingine vya michezo na kusema wanapokea kwa mikoni miwili vifaa hivyo.

Tangu ateuliwe Naibu Katibu Mkuu Methusela Ntonda hii ni ziara ya pili hapa MCSD.


No comments:

Post a Comment