Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati, Mchungaji Dkt. Syprian Hilinti (kushoto) akizungumza katika harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa hilo Usharika wa Chungu lililopo Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu
Wachungaji wa kanisa hilo wakiwa kwenye harambee hiyo.
Waumini wakiwa kwenye harambee hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Ikungi
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu amechangia saruji mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chungu lililopo Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida.
Kingu ametoa msaada huo wakati wa harambee iliyofanyika katika kanisa hilo leo hii ambayo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Kati, Mchungaji Dkt. Syprian Hilinti.
Aidha katika harambe hiyo Kingu alichangia kutengeneza madirisha yote ya nyumba ya mchungaji wa ushirika huo.
Akizungumza katika harambee hiyo Mchungaji Dkt.Syprian Hilinti alimshukuru Mbunge Kingu na kumuombea kwa Mungu kutokana na mchango wake huo mkubwa kwa kanisa.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kumuelezea kuwa ni mtu anayejitoa kusaidia shughuli nyingi za kijamii na misaada ya ujenzi wa makanisa na misikiti katika jimbo hilo.
"Kingu amekuwa akijitoa sana kuchangia shughuli za maendeleo na kuchangia ujenzi wa makanisa na misikiti hakika Jimbo la Singida Magharibi tumepata mbunge,". alisema muumini wa kanisa hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake.
No comments:
Post a Comment