MAINJINIA VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 26 August 2021

MAINJINIA VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema akizungumza na wahandisi vijana jana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).


Msajili wa Wahandisi, Eng. Patrick Barozi akizungumza na wahandisi vijana jana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na ERB.


Baadhi ya wahandisi vijana wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na ERB.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema akizungumza na wahandisi vijana jana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).


Sehemu ya washiriki wakiwa kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na ERB.jana jijini Dar es Salaam 

Msajili wa Wahandisi, Eng. Patrick Barozi akisisitiza jambo alipozungumza na wahandisi vijana jana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na ERB.

MWENYEKITI wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema amezungumzia umuhimu wa wahandisi vijana kubuni teknolojia mpya zitakazowiana na mahitaji ya dunia ya sasa. Amesema kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ari ya kutatua changamoto itasaidia dunia kuwa na ufumbuzi na maendeleo endelevu.

Prof. Lema ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la wahandisi vijana huku akiwataka wahandisi vijana kubaini changamoto za kihandisi na kutumia fursa zilizopo kuharakisha maendeleo yatakayokuza taaluma yao na uchumi wa nchi.

"Tumikieni jamii kwa juhudi, uadilifu na maarifa ili kuleta maendeleo na jamii haitawatupa," amesema Prof. Lema.

Msajili wa Wahandisi, Eng. Patrick Barozi amesema kongamano hilo ni sehemu ya mkakati wa ERB kuwaweka pamoja wahandisi vijana kujadiliana kuhusu shughuli za wahandisi na kubadilishana uzoefu na kubaini fursa zilizopo katika taaluma yao.

Amesema zaidi ya wahandisi elfu thelathini na moja wamesajiliwa na ERB hapa nchini hivyo watumie wingi wao kuleta mapinduzi ya kweli kiuchumi, kiteknolojia na kimiundombinu nchini kote.

Ameishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuhamasisha wanawake kujiunga na fani ya uhandisi ambapo takriban wahandisi 756 wamesajiliwa na bodi hiyo toka 96 waliokuwepo mwaka 2010.

Amewataka wahandisi vijana kuhamasisha wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kusoma masomo ya sayansi ili kujakuwa wahandisi watakapofika vyuo vikuu.

Kongamano la wahandisi vijana ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wahandisi nchini yatakayoanza rasmi septemba 2, mwaka huu jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine wahandisi hao watakagua miradi ya ujenzi inayoendelea nchini kuona kazi za kihandisi zinavyofanyika.

Baadhi ya wahandisi vijana wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano la wahandisi vijana lililoandaliwa na ERB.



No comments:

Post a Comment