VIPINDI VYA UPEPO MKALI WA KUSI VINATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI, TMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 1 June 2021

VIPINDI VYA UPEPO MKALI WA KUSI VINATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI, TMA

 

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi 

MWENENDO WA UPEPO KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI (JJA), 2021

KWA kawaida msimu wa kipupwe hutawaliwa na upepo wa Kusi. Kutokana na matarajio ya uimarikaji wa wastani wa mgandamizo mkubwa wa hewa kusini mwa Afrika vipindi vichache vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza. Hata hivyo, katika kipindi cha miezi ya Juni na Agosti, 2021 vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. 

Zaidi ya hapo, katika msimu wa mwaka huu, vipindi vya upepo unaovuma kutoka kusini-mashariki na mashariki

(Matlai) vinatarajiwa katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi na maeneo ya mwambao wa pwani hususan mwezi June, 2021. Hali hii inatarajiwa kuleta unyevunyevu kutoka katika bahari ya Hindi na kusababisha vipindi vifupi vya mvua nyepesi katika maeneo machache ya visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na ukanda wa Pwani (Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara). 

Aidha, katika ukanda wa Ziwa Victoria vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo machache.

4.0 ATHARI NA USHAURI

Hali ya baridi inayotarajiwa hususan maeneo yenye miinuko ya Nyanda za juu Kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe), inaweza kuleta athari kwa binadamu, wanyama, samaki pamoja na ustawi wa mazao mashambani hususani mazao ya muda mrefu kama migomba yanaweza kupata magonjwa ya fangasi na kudhoofisha ustawi wake. Kutokana

na hali ya joto katika bahari ya Hindi kuwa juu ya wastani, ongezeko la tija katika shughuli za uvuvi katika kipindi cha msimu huu linatarajiwa.

Hali ya ukavu na upepo inaweza kuongeza upotevu wa maji kwa njia ya mvukizo na kuathiri upatikanaji wa maji kwa mazao, mifugo na matumizi mengine. Hivyo, Jamii inashauriwa Page 6 of 6 727K –00/2020 kuchukua hatua za tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi mazuri ya maji na kujikinga ili kupunguza athari mbaya zinazoweza kusababishwa na hali ya hewa inayotarajiwa.

Mwelekeo wa hali ya hewa uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya hewa katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10 pamoja na mwezi kama unavyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya

hewa na kutoa taarifa.

Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania: 

No comments:

Post a Comment