Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga amesema wafanyabiashara hawana budi kuhakikisha mahindi wanayonunua kama yamezingatia kanuni bora za kulimo ili kuzuia fangasi wanaoweza kusababisha sumu kuvu kwenye mahindi.
Alisema wafanyabiashara hao wanatakiwa kujua mahindi wanayokuwa wakinunua yanayotoka wapi ili kuweza kuepuka hasara inayoweza kujitokeza pindi mahindi yatakapokuwa na sumu kuvu.
"Ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kujua Mahindi wanayoyanunua yanazalishwaje kwani ni muhimu sana kujua yule anayekuuzia mahindi kwa lengo la kujua kama anafuata kanuni bora za kilimo kutokana na kwamba inakupa uhakika na ukinunua haitaleta shida kwenye usafirishaji,"alisema Msasalaga.
"Mafunzo haya yatawasaidia wafanyabiashara namna ya mahindi yanavyopokelewa,kuna taratibu za kupeleka mahindi nje ya Nchi na kila Nchi ina namna ya kulinda usalama wa wananchi wake," alisema Msasalaga.
Akielezea namna ya sumu kuvu iweze kuepukika,Msasalaga amesema ni lazima kanuni bora za usindikaji wa mahindi na mnyonyoro mzima wa uzalishaji uwe umefuatwa huku akiwataka wafanyabiashara wafuate taratibu ambazo zinatakiwa kwa kuwa nchi inayopokea bidhaa ndio inayotoa sharti ya kupokea mizigo.
Semina hiyo inafanyika katika Mikoa mitatu yenye Mipaka ya Holili mkoani Kilimanjaro,Namanga Mkoani Arusha na Horohoro Mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment