SONGWE KUONGEZA UKAGUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 30 June 2021

SONGWE KUONGEZA UKAGUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea akizungumza na wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe wakati wakipewa mafunzo yaliyo endeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

MKOA wa Songwe umeweka msisitizo katika Ukaguzi wa Madawa na vifaa tiba ili kudhibiti dawa na vifaa tiba ambavyo havipo sokoni au havija sajiliwa kuwafikia watumiaji.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa dawa na vifaa tiba wa halmashauri zote za Mkoa wa Songwe ambapo mafunzo hayo yameendeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Dkt Nyembea amesema Mkoa wa Songwe unapakana na Nchi mbalimbali na hivyo kuwa na njia ambazo si rasmi zinazotumiwa na wahalifu kuingiza nchini Dawa na Vifaa tiba ambavyo havijasajiliwa au havipo.

“Mafunzo haya yatasaidia kuimarisha ukaguzi wa dawa na vifaa visivyofaa visizagae sokoni na hivyo kuleta madhara kwa watumiaji”., Dkt Nyembea.

Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Anitha Mshigati amesema katika mafunzo hayo wakaguzi watakumbushwa maadili ya Ukaguzi ili waweze kuboresha kazi hiyo kwa kufuata taratibu na sharia na matarajio ni kuwa baada ya mafunzo kazi hiyo itafanyika na kuleta tija zaidi.

Naye Mtaalamu wa Maabara wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Ashura Mwinyimkuu amesema changamoto wanazo kutana nazo ni jamii kutokuwa na elimu kuhusu ukaguzi hivyo kushindwa kutoa ushirikiano na mafunzo waliyopata yamewaongezea ujuzi wa namna ya kukabiliana na hilo.

Kwau upande wake Mfamasia  wa Songwe Medard Mwazembe amesema changamoto ya wakaguzi ni ukubwa wa maeneo ya kufanya ukaguzi huku wakiwa hawana vifaa vya usafiri hivyo wanaomba TMDA kwa kushirikiana na Mkoa kutoa elimu kwa viongozi wa Kijiji na Kata ili viongozi hao waweze kusaidia kutoa elimu katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment