|
Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakipata picha ya kumbukumbu na walimbwende hao maarufu Faraja Kota Nyalandu aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 huku Nancy Sumari, mrembo wa Tanzania mwaka 2005 na Mrembo wa Dunia wa Afrika kwa mwaka 2005 mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao. |
|
Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha kuwa balozi wa elimu Mwanamitindo Flaviana Matata mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) kilichotolewa na TEA kutambua mchango wa mrembo huyo kwenye sekta ya elimu. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania Prof. Maurice Mbago. |
|
Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha kuwa balozi wa elimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja Kota Nyalandu. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania Prof. Maurice Mbago. |
|
Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga akizungumza kwenye Kongamano la Wadau na Wachangiaji wa Elimu lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kufanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). |
|
Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Waziri Salum akizungumza kwenye kwenye hafla ya Kongamano la Wadau na Wachangiaji wa Elimu lililoandaliwa na TEA na kufanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bahati Geuzye akizungumza kwenye kwenye hafla ya Kongamano la Wadau na Wachangiaji wa Elimu lililoandaliwa na TEA na kufanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). |
|
Wadau na Wachangiaji wa Elimu wakiwa kwenye kongamano hilo lililoandaliwa na TEA Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). |
|
Faraja Kota Nyalandu (kulia) akiwa kwenye mjadala kwenye hafla ya Kongamano la Wadau na Wachangiaji wa Elimu. |
WAREMBO Faraja Kota na Mwanamitindo Flaviana Matata mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) wametangazwa rasmi kuwa mabalozi wa elimu na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Walimbwende hao maarufu Faraja Kota Nyalandu aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 huku Mwanamitindo Flaviana Matata mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) wamepewa heshima hiyo na TEA kwenye hafla ya Kongamano la Wadau na Wachangiaji wa Elimu lililoandaliwa na taasisi hiyo.
Kabla ya kupewa heshima hiyo Mamlaka ya Elimu Tanzania iliwapa cheti maalum cha kutambua mchango wao kwenye sekta ya elimu pamoja na taasisi nyingine zinazojitolea kuchangia elimu ikiwemo pia Benki ya NMB.
Kongamano hilo la kwanza la TEA lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lilikutanisha wadau mbalimbali wanaojitoa kwa namna moja ama nyingine kuchangia elimu nchini.
Faraja Kota Nyalandu ambaye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Shule Direct inayowasaidia wanafunzi hasa wa sekondari kufundisha mada mbalimbali kupitia teknolojia ya mtandao amekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi na walimu, huku Mwanamitindo Flaviana Matata mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa kupitia taasisi yake (FMF) amekuwa akisaidia na kufadhili wanafunzi kimasomo na misaada ya ujenzi na ukarabati miundombinu ya elimu katika shule kadhaa nchini.
No comments:
Post a Comment