Wahudumu wa kituo cha huduma kwa wateja 'TPA call center' jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi. |
Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Bw. Erick Hamis akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja 'TPA call center' jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja 'TPA call center' jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (katikati) akitoa maelekezo alipokagua kituo hicho cha huduma kwa wateja 'TPA call center' mara baada ya kukizindua. |
Dkt. Chamuriho amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kituo cha huduma kwa mteja TPA Call Center kitakachotoa msaada na taarifa muhimu kwa wateja wanaoagiza bidhaa, kutafuta masoko na kusafirisha bidhaa sehemu mbalimbali duniani.
“Kukamilika kwa ujenzi wa gati namba 1-7 katika bandari ya Dar es salaam, kuboreshwa kwa ujenzi wa bandari za Tanga na Mtwara kunaongeza changamoto ya kuongeza wateja wa bandari hizo hivyo hakikisheni kituo hicho kinatatua kero za wateja na hivyo kuwavutia kutumia bandari za Tanzania”, amesema Waziri Dkt. Chamuriho.
Waziri Dkt. Chamuriho ameipongeza TTCL kwa kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho kwa wakati na kuitaka TPA kujibu changamoto za wateja kwa wakati na kufanya kazi kwa saa 24, ili kuvutia wateja na kuleta tija kwenye bandari za Tanzania.
“ Namba ya simu itakayotumika katika Kituo hicho ni 0800110032 ambayo itakuwa bure kwa mitandao yote”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Prof. Ignas Rubaratuka amesema uzinduzi huo utaongeza ufanisi wa bandari zinazosimamiwa na TPA na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania Bwana, Erick Hamis amesema uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya mkakati mkubwa wa TPA kuvutia wateja na kutoa huduma zenye ubora katika bandari zake zote hapa nchini.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI.
No comments:
Post a Comment