BINGWA WA MADARAJA MHANDISI MFUGALE AFARIKI DUNIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 30 June 2021

BINGWA WA MADARAJA MHANDISI MFUGALE AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale.


WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi inasikitika kutangaza kifo cha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale, kilichotokea leo tarehe 29 Juni, 2021.

Mhandisi Patrick Mfugale, amefariki dunia majira ya saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Taratibu za mazishi ya marehemu Mhandisi Mfugale zinapangwa na zitatangazwa hapo baadaye kwa kushirikiana na familia ya marehemu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe, Amina.

Imetolewa na; Mhandisi Joseph Malongo

Katibu Mkuu (Ujenzi)

Dodoma

29 Juni, 2021

No comments:

Post a Comment