WAZIRI WA FEDHA DKT. MWIGULU NCHEMBA NA NAIBU WAKE MHANDISI HAMAD MASAUNI WAANZA KAZI RASMI BAADA YA KUAPISHWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 1 April 2021

WAZIRI WA FEDHA DKT. MWIGULU NCHEMBA NA NAIBU WAKE MHANDISI HAMAD MASAUNI WAANZA KAZI RASMI BAADA YA KUAPISHWA


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck  Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea shada la maua alipowasili  katika Ofisi za Wizara  zilizopo Mji wa Kiserikali wa Magufuli -Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Bi. Emiliana Shayo, alipowasili  katika Ofisi za Wizara  zilizopo Mji wa Kiserikali wa Magufuli -Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu  Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika kikao cha menejimenti ya wizara katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment