WAZIRI BASHUNGWA AOMBA USHIRIKIANO KWA BALOZI WA EU KWA ‘RESALE RIGHT’ KAZI ZA SANAA YA UFUNDI KATIKA NCHI ZA ULAYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 17 March 2021

WAZIRI BASHUNGWA AOMBA USHIRIKIANO KWA BALOZI WA EU KWA ‘RESALE RIGHT’ KAZI ZA SANAA YA UFUNDI KATIKA NCHI ZA ULAYA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa akifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Manfredo Fanti leo Machi 17, 2021 Jijini Dar es Salaam ambapo amemweleza maombi ya Ushirikiano na nchi za Ulaya katika masuala ya ‘resale right’ katika kazi za Sanaa ya ufundi.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa (wasaba kulia) akiwa katika picha ya pamoja na na Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Manfredo Fanti (watano kushoto) leo Machi 17, 2021 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo  yaliyolenga mashirikiano katika sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wakurugenzi wa kiseka wa Wizarani na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo, wa pili kuchoto ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare.


Anitha Jonas – COSOTA , Dar es Salaam

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa leo Machi 17,2021 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania na Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti aambapo amemwomba   ushirikiano  katika nchi za Ulaya katika   kazi za Sanaa ya Ufundi za Wasanii  wa nchini kunufaika na mauzo ya kazi zao zinapouzwa katika nchini hizo kupitia  minada mikubwa kwa kulingana na Kanuni  ya 'resale  right' inayosimamiwa na Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA).

 

 Akiendelea na mazungumzo hayo Waziri Bashushwa alimweleza balozi huyo  kuwepo kwa changamoto kwa Sanaa ya Tingatinga nchini ya kurubuniwa katika mikataba mbalimbali mauzo yake ya saana yake ambapo imeleta changamoto ya suala la Hakimiliki, ambapo changamoto hiya mikataba hiyo inafanyiwa kazi na COSOTA hivi sasa.

 

 Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Mhe.Bashungwa aliezea Taasisi ya Hakimiliki Tanzania chini ya Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bibi. Doreen Sinare imekuwa ikilifuatulia suala hilo, kufuatia mikataba mibovu waliyoingia na kampuni mbalimbali.. 


‘Ushirikiano huu utaleta chachu katika utatuzi wa uhitaji wa masoko ya uhakika kwa kazi za Sanaa ya Ufundi na kuchangia kukua kwa Sanaa hii ambayo wasanii wataifa hili wanaifanya vizuri ,’alisema Mhe.Bahungwa.

 Aidha, Waziri Bashungwa alieleza juu ya mashirikiano na COSOTA, jitihada za serikali katika kuimarisha taasisi hiyo iliiweze kufanya majukumu yake vyema hususan katika kulinda kazi za Sanaa hasa muziki na kuongeza kipato kwa wasanii na Wabunifu  sababu ni moja ya taasisi yenye tija na maslahi mapana ya taifa na yenye dhamana ya kulinda hakimili nchini. 

 

 Katika mazunguzo hayo Waziri huyo amesisitiza  mashirikiano katika Taasisi za COSOTA, TASUBA na Chuo cha Malya. Mazungumzo hayo kati ya Balozi huyo na Waziri yalifanyika mbele ya Wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo kwa lengo la kila mmoja kueleza maeneo ya taasisi yake  ambayo angependa kushirikiana na ubalozi huo.

 

Kwa upande wa Balozi wa huyo wa Umoja wa Ulaya nchini Bw.Manfredo Fanti alieleza dhamira yake ya kutoaushirikia katika sekta hizo kwa kuomba baadhi ya watendaji wake kukutana na viongozi hao wanaosimamia sekta ya habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa lengo la kujipanga vyema namna wanavyoweza kufanya kazi katika maeneo yao.


No comments:

Post a Comment