WANANCHI DAR WAANZA KUMUAGA HAYATI DK. MAGUFULI, VILIO, SIMANZIVYATAWALA, WAZIMIA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 21 March 2021

WANANCHI DAR WAANZA KUMUAGA HAYATI DK. MAGUFULI, VILIO, SIMANZIVYATAWALA, WAZIMIA...!

Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli wakati wakitoka Ikulu jijini Dar es Salaam na kuelekea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay kwa ajili ya Misa ya kumuombea Marehemu.


Wajasiriamali wa Mau wa Namanga mkoani Dar es Salaam wakirusha maua kama ishara ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi mkoani Dar es Salaam.


Wajasiriamali wa Mau wa Namanga mkoani Dar es Salaam wakirusha maua kama ishara ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi mkoani Dar es Salaam.


Wakazi wa Biafra Kinondoni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa 


Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli ukiwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay mara baada ya kuwasili.


Waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay wakilia wakati Jeneza lenye mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli ulipokuwa ukitolewa Kanisani hapo.


Wananchi wa Kinondoni Mkwajuni na Magomeni Morocco wakiwa wamesimama barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa kuelekea Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.


Wakazi wa Biafra Kinondoni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa 


Wakazi wa Kinondoni, Magomeni , Kigogo, Msimbazi Center na Karume wakiwa wamesimama kando ya barabara kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Wakazi wa Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Msimbazi Center na Karume wakiwa wametandika kanga barabarani na kusimama kando ya barabara kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Wakazi wa Kigogo, Msimbazi Center na Karume, Mataa ya Chang’ombe wakiwa wamesimama kando ya barabara kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Wengine barabarani walilia huku wakipunga majani kuashiria kumuaga kipenzi huyo na jemedari wa Watanzania.

Na Joachim Mushi, Dar

VIONGOZI na baadhi ya Wananchi leo jijini Dar es Salaam wameanza kutoa heshima za mwisho kwa Hayati, Dk. John Pombe Magufuli huku shughuli hiyo ikitawaliwa na vilio, simanzi, majonzi na heshima ya kipekee kupewa mwili wa shujaa huyo wa Tanzania na Afrika.

Vilio vilianza kutawala katika ibada takatifu asubuhi iliyofanyika Kanisa Katoliki la St. Peter jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili mwili wa Hayati Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuombewa kabla ya mwili huo kupelekwa Uwanja wa Uhuru, ambapo ilifanyika ibada nyingine ya kumuombea na baadaye viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.

Mwili wa Hayati Dk. Magufuli ukiwa njiani kuelekea uwanja wa Uhuru wananchi walijitokeza barabarani huku wengine wakitandika nguo kama kanga barabarani unapopita kuonesha heshima na upendo wa kipekee kwa kipenzi chao. Wananchi baadhi walisikika wakipiga mayowe ya vilio na semi mbalimbali ya kumkumbuka kiongozi huyo na kipenzi cha wengi.

Maeneo mengine wananchi walishindwa kujizuia na kulisogelea zaidi gari lililobeba mwili wake huku wakitamani kuligusa ikiwa ni ishara ya kuguswa na kuumia kwa msiba huo. Hakika Hayati Dk. Magufuli alikuwa Rais na kipenzi cha wengi hasa wanyonge maana wengine walisimama barabarani na matawi ya miti wakimpungia kuonesha ishara ya kumuaga.

Mwili wa Hayati Dk. Magufuli ukipita eneo la Mbuyuni ukitokea Kanisa Katoliki la St. Peter kuelekea uwanja wa Uhuru ulikumbana na maua ya rangi mbalimbali yakirushwa barabarani na kwenye gari lililobeba mwili wake na wauza maua wa eneo hilo ikiwa ni ishara ya kumuaga na kuguswa na msiba huo. Ama kweli Watanzania na hasa wanyonge wameumia na kujeruhiwa kwa msiba wa kiongozi huyo shupavu.

Wakiaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Magufuli uwanja wa Uhuru, vilio na hata kuzimia kwa baadhi ya wananchi walioshindwa kujizuia ilikuwa matukio ya kawaida. Watu wa msalama mwekundu na askari walikuwa na kazi ya ziada kuwasaidia wananchi pale walipozidiwa. Hali hiyo uliendelea pia jioni mwili wa mpendwa Dk. Magufuli ulipokuwa ukirejeshwa Lugalo kuhifadhiwa baada ya shughuli za heshima za mwisho.

Bila kujali usiku wananchi waliacha shughuli zao na kusimama barabarani wakiuaga mwili huo ulipokuwa ukipita kuelekea Hospitali ya Jeshi ya Lugalo. Makundi mengine ya wananchi walisikika wakiimba nyimbo za maombolezo na kupaza sauti kumuaga kipenzi chao. 

Wafanyabiashara ndogo ndogo, mama lishe na wamachinga walilazimika kuacha shughulizao na kusogea pembezoni mwa barabara kumuaga Dk Magufuli. Ama kweli msiba huo umegusa na kuwaliza wengi, Pumzika Baba, Pumzika Jembe, Pumzika Baba Magufuli mwendo umeumaliza na alama umeacha. Amina.

No comments:

Post a Comment